Mikopo 193 yafungua milango ya ajira 820 kwa vijana

HomeKitaifa

Mikopo 193 yafungua milango ya ajira 820 kwa vijana

Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) imetoa mikopo 193 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 820, hatua iliyosaidia kuzalisha ajira nyingu nyingi kwa vijana.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Judith Kapinga leo Januari 24, 2026, wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa siku 100 za Ahadi ya Serikali ya Awamu ya Sita katika sekta ya viwanda na biashara.

Amesema katika kipindi hicho, maelfu ya kampuni, majina ya biashara pamoja na leseni za viwanda zinazomilikiwa na vijana zimesajiliwa ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika uchumi wa nchi.

error: Content is protected !!