Suala la kuadimika kwa mipira ya kiume (kondomu) limezua mjadala mkali kwenye Baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, ambapo Madiwani hao wamedai linakwamisha mapambano dhidi ya UKIMWI.
Wakizungumza wakati wa baraza hilo mjini Iringa madiwani hao wamedai kuwa hivi sasa mipira hiyo haipatikani kwenye nyumba za wageni na maeneo ya starehe yaliyopo kwenye kata zao, hali waliyosema inaweza kuongeza maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI.
Mkoa wa Iringa ni wa pili nchini kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi ya UKIMWI, ukitanguliwa na mkoa wa Njombe.