Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani, WHO, Kanda ya Afrika, Dkt. Mohamed Janabi amesema Tanzania imepiga hatua katika kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano kutoka 81 hadi 68 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa hai kati ya mwaka 2015 na 2022.
Dkt. Janabi ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa jengo la kisasa la kuhudumia watoto njiti katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, akisisitiza kuwa uwekezaji katika huduma za watoto wachanga ni muhimu zaidi katika kuokoa maisha.
Amesema watoto njiti ni miongoni mwa walio hatarini zaidi, hivyo miundombinu bora na wataalamu waliobobea ni sehemu ya suluhisho la kupunguza vifo vinavyozuilika.
Jengo hilo limejengwa na Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, likilenga kuimarisha huduma za mama na mtoto katika Kanda ya Ziwa.



