TTCL, Posta zaandika historia uchangiaji gawio serikalini

HomeKitaifa

TTCL, Posta zaandika historia uchangiaji gawio serikalini

Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na Shirika la Posta Tanzania zimeandika historia mpya baada ya kurejea katika faida na kuanza kuchangia gawio serikalini, hatua inayoonesha kuimarika kwa ufanisi wa taasisi hizo za umma.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa leo Ikulu Dar es Salaam katika hafla ya kupokea gawio kutoka kwa mashirika na taasisi za umma mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan, Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu alisema TTCL imepata faida ya shilingi bilioni 22.9 na kutoa gawio la shilingi bilioni 1.6 kwa Serikali. Mwaka wa fedha uliopita, kampuni hiyo ilirekodi hasara ya shilingi bilioni 18.

Kwa upande wa Shirika la Posta Tanzania, limepata faida ya shilingi bilioni 2.8 na pia kutoa sehemu ya faida hiyo kama gawio kwa Serikali.

error: Content is protected !!