Rais Samia: anayeharibu mali za umma ni adui ni adui wa taifa

HomeKitaifa

Rais Samia: anayeharibu mali za umma ni adui ni adui wa taifa

Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amewaonya watu wenye tabia ya kuharibu kwa makusudi mali za umma ikiwemo miundombinu ya barabara,wanahujumu maendeleo kwani serikali inatumia miaka mingi kutafuta fedha za ujenzi wa miundombinu hiyo.

Amesisitiza kuwa mtu yoyote atakayeharibu mali za umma anateketeza fedha za wananchi, kuhujumu uchumi na kurudisha nyuma maendeleo ya taifa hivyo mtu huyo ni adui wa taifa huku akiiasa jamii kuwa walinzi namba moja wa miundombinu hiyo.

Ametoa kauli hiyo hii Agosti 7,2026 katika hafla ya ufunguzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo kasi awamu ya pili iliyofanyika Temeke kwa Azizi Ally Mkoani Dar es Salaam.

error: Content is protected !!