Jeshi la Polisi mkoani Tabora limewataka wananchi kusalimisha silaha haramu katika kipindi cha siku 18 zilizobaki ili kuepuka kuchukuliwa hatua kali za kisheria baada ya kumalizika kwa kipindi cha msamaha.
Hayo yamesemwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ambae pia ni Mkuu wa Polisi Jamii mkoani Tabora, Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP) Mahemba Kavalambi leo Oktoba 14, 2026 wakati akizungumza na Vyombo vya Habari mkoani humo.
ACP Kavalambi amesema, baada ya kumalizika kwa kipindi cha Msamaha wa Usalimishaji wa Silaha haramu kwa hiari, Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora litafanya msako mkali wa kuwatafuta na kuwabaini wale wote ambao wanamiliki silaha kinyume cha Sheria.


