Serikali kuwezesha wahitimu 10,000 kupata mafunzo ya uzoefu wa kazi kila mwaka

HomeKitaifa

Serikali kuwezesha wahitimu 10,000 kupata mafunzo ya uzoefu wa kazi kila mwaka

Serikali imesema imeandaa Mpango wa Taifa wa Mafunzo ya Uzoefu wa Kazi kwa Wahitimu (2026/27 – 2030/31) unaolenga kuwezesha wahitimu 10,000 kila mwaka kupata mafunzo ya uzoefu wa kazi (Internship).

Akijibu swali bungeni, Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Dkt. Evaline Munisi amesema lengo la mpango huo ni kupunguza pengo kati ya ujuzi unaotolewa na taasisi za elimu na mafunzo na mahitaji ya soko la ajira la ndani na nje ya nchi.

Aidha, ameeleza kuwa Serikali imeandaa Mwongozo wa Taifa wa Mafunzo kwa Vitendo kwa Wahitimu wa mwaka 2017 unaotumika katika sekta ya umma na binafsi.

“Tangu kuanza utekelezaji wa programu hii mwaka 2017/18 hadi Septemba 2026, Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imewezesha wahitimu 34,549 kupata mafunzo ya uzoefu wa kazi.

Ameongeza kuwa kati ya wahitimu hao, wahitimu 11,263 wameajiriwa baada ya kukamilisha mafunzo yao na wahitimu 5,116 wameanzisha shughuli za kujiajiri.

 

error: Content is protected !!