Serikali kununua ndege 5 za mafunzo ya urubani

HomeKitaifa

Serikali kununua ndege 5 za mafunzo ya urubani

Serikali imesema Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kitanunuliwa ndege tano za mafunzo ya urubani kuanzia mwaka huu wa fedha.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara amesema hayo wakati wa zaira ya kikazi kwenye Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Dar es Salaam.

Waitara amesema hayo baada ya Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari kumweleza kuwa kwa sasa mamlaka hiyo inawaepeleka wanafunzi kwenye chuo cha urubani cha Uganda kwa kuwa NIT hakijakidhi vigezo ikiwa pamoja na kupata ithibati sambamba na kuwa na ndege za mafunzo.

Akijibu hoja hiyo, Waitara amesema Serikali ya Awamu ya Tano iliahidi kuinunulia NIT ndege mbili za mafunzo ya urubani na tayari NIT walishapewa zaidi ya bilioni 3 za malipo ya awali.

error: Content is protected !!