Balozi mdogo wa Sudan nchini Urusi ameashiria baadhi ya marekebisho katika makubaliano ya kijeshi kati ya nchi yake na Russia.
Anwar Ahmed Anwar, balozi wa Sudan nchini Urusi amesema nchi yake haihitaji msaada wa kiuchumi kutoka Urusi mbali na mkataba wa makubaliano wa kuanzishwa vituo vya lojistiki ya jeshi la wanamaji la nchi hiyo katika bandari ya Sudan.
Kabla ya hapo jeshi la Sudan limelieleza shirika la habari la Sputnik kwamba, Khartoum inataka marekebisho yafanyike katika mkataba wa makubaliano wa mwaka 2020 kuhusu ujenzi wa vituo vya kilojstiki vya jeshi la wanamaji la Urusi katika bandari ya Sudan na itaiomba Moscow msaada au pengine kuingia nayo mkataba wa kiuchumi wa kuikodisha bandari hiyo kwa muda wa miaka mitano.
Mazungumzo kati ya Urusi na Sudan kuhusiana na ujenzi wa kituo cha lojistiki cha baharini yalianza mwaka 2017 wakati aliyekuwa rais wa Sudan, Omar Al Bashir alipoeleza kwamba amependekeza wazo hilo kwa Rais Vladimir Putin wa Urusi na waziri wa ulinzi wa nchi hiyo, Jenerali Sergey Shoygu.