Kesi ya Mbowe kuanza kusikilizwa leo

HomeKitaifa

Kesi ya Mbowe kuanza kusikilizwa leo

Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, leo inatarajiwa kuanza kuwasikiliza mashahidi wa upande wa Jamhuri katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Mbowe na wenzake watatu wanatarajia kupanda kizimbani mbele ya Jaji Mustafa Siyani, wakati shauri hilo litakapopelekwa kwa usikilizwaji.

Kesi hiyo inaanza kusikilizwa baada ya upande wa Jamhuri kuwasomea washtakiwa hao maelezo ya awali, ambapo walikubali taarifa zao binafsi tu.

Wakati wa usikilizwaji huo, upande wa Jamhuri unatarajia kuita mashahidi 24 na vielelezo 19, ili kuthibitisha mashitaka dhidi ya washitakiwa hao.

Upande wa utetezi unatarajiwa kuwa na mashahidi 11 ambao wanne kati yao hawakutajwa majina wala anwani zao kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na sababu za kiusalama.

error: Content is protected !!