Mambo 5 muhimu ya kufanya kabla ya kulala

HomeElimu

Mambo 5 muhimu ya kufanya kabla ya kulala

1. Panga mambo ya siku ifuatayo
Kabla ya kulala, tumia dakika tano au kumi kupitia mipango yako. Andika orodha ya mambo yote unayoyahitaji kuyaanya, (mfano kuandika ripoti zako za kazi au ratiba za kuhudhuria mkutano), kisha andika orodha ya mambo ambayo ungependa kutimiza kwanza, (mfano muda wa mazoezi au kusafisha nyumba). Ikiwa orodha inakuwa ndefu sana, ainisha vipaumbele na kuanza navyo na vingine ufanye siku nyingine za wiki kutokana na ratiba yako. Kwa kufanya haya kabla ya kulala, utaamka asubuhi ukijua ni nini kinahitajika kufanyika hivyo utajua wapi pa kuanzia siku.

2. Fanya usafi wa nyumba au chumba chako
Ujanja mwingine mzuri ni kusafisha nyumba yako na mazingira yanayoizunguka nyumba yako. Hakikisha unasafisha vyombo jikoni viwe safi ili unapoamka asubuhi iwe rahisi kutumia na sio kuanza kuviosha. Usisahau pia kuweka kila kitu sehemu yake kwa mfano viatu na nguo. Kwa watu wengine, ni wakati mzuri wa kuandaa nguo za kuvaa na kuweka sehemu sahihi ili unapoamka uvitumie.

3. Itafakari siku yako na kuweka sawa akili yako
Lengo halisi la kutafakari ni kukuza ubora wa afya, upendo, amani, uwepo mzuri ambao unaweza kuendelea kwa kila siku katika shughuli za maisha yako. Kila kipindi kifupi cha kutafakari kwa utulivu hugusa na kukuza nguvu zako na kukupa njia ya kutatua changamoto zako na kujua wapi pa kuanzia unapoamka kwenda kutekeleza majukumu yako ya kila siku.

4. Andaa nguo zako na vifaa vya mazoezi
Njia nzuri ya kuanza siku ni kufanya mazoezi, kama vile kukimbia, kutembea au kuendesha baiskeli. Pia kuandaa nguo zako za kwa ajili ya siku inayofuata ni muhimu kwa sababu utaokoa muda unapoamka kwenda katika shuguli zako za kila siku. Inachukua dakika tano tu kuandaa nguo zako na via vifaa vya mazoezi kabla ya kulala, badala ya kuhangaika asubuhi unapoamka.

5. Zima simu yako
Kufurahia usingizi wako vizuri kila ifikapo usiku ni muhimu kuzima simu ikiwa unataka kutimiza majukumu yako vyema siku inayofuata. Kuepuka haya zima simu yako au ondoa sauti. Kumbuka, simu, barua pepe na taarifa za kawaida zinaweza kusubiri hadi asubuhi. Na ikiwa unapata usingizi mzuri wa usiku, utaweza kushughulikia ujumbe wowote kwa njia nzuri na yenye ufanisi zaidi.

error: Content is protected !!