– Ina umbo jembamba ambalo utafiti unaonesha watu wengi wanapenda simu nyembemba kwa sasa.
– Kioo chake kina teknolojia mpya aina ya ‘Ceramic’ ambapo ndio itakuwa simu yenye kioo imara zaidi kuliko simu nyingine dhidi ya kuanguka na kuchubuka.
– Iphone 13 kioo chake hakiruhusu maji na umbile lake kwa pembeni limewambwa kwa aluminiam.
– Unaweza kupata iPhone 13 kati rangi 5 tofauti, ambazo ni nyekundu, pinki, bluu, nyeusi na nyeupe.
– Ili kulinda mazingira, “material” kutoka kwenye chupa cha plastiki zilizorejeleshwa (recycled bottles) ni miongoni mwa “material” yalizotumika kuunda umbo la nje la iPhone 13
– Apple wametoa matoleo manne ya iPhone 13 ambayo ni iPhone 13, iPhone 13 Mini, iPhone 13 Pro na iPhone 13 Pro Max ambapo zote zina tabia za kufanana.
– Zaidi ya asilimia 90% ya umbo la iPhone 13 limeigwa kutoka kwa iPhone 12. Hivyo kwa kuzitazama hakuna tofauti kubwa.
– Uwezo wa betri kukaa na chaji umeongezwa, kutoka saa moja na nusu mpaka saa mbili kwa nusu kama utatumia mfululizo.
– iPhone 13 imeboreshwa Camera zaidi. Inaweza kupiga picha pana zaidi (ultra wide lens), na yenye mwanga mzuri hata katika eneo lenye mwanga mdogo.
– iPhone 13 imewekewa uwezo wa kasi ya 5G kwenye kuperuzi.
– iPhone 13 imewekewa uwezo wa ‘Cinematic Mode’. Yaani imepewa uwezo kama Camera zinazotumika kwenye kurekodi filamu.
– Unaweza kupiga picha/video ukaihariri (edit) hapo hapo na kuituma bila kupungua ubora. Inauwezo wa kuhamisha ‘focus’, yaani kufanya akili na macho yako kuhama kulingana na uelekeo wa camera katika picha.
– Super Retina XDR Display, inafanya iPhone 13 kuwa simu yenye kasi zaidi katika kuchakata mafaili, kutafuta na muonekano mzuri zaidi.