Uonapo ishara hizi 4, badili tairi za gari yako

HomeElimu

Uonapo ishara hizi 4, badili tairi za gari yako

Maisha yetu yana mihangaiko sana, kiasi cha kukosa muda kutazama usalama wa mazingira yetu.

Ni nani hutazama tairi za gari lako kujua kama bado ni salama kutumika? Hizi ni sababu kubwa nne kwanini ubadilishe tairi zako:

1. Kuvimba kwa sehemu ya tairi
Athari ya kuvimba kwa tairi husababishwa kwa gari kupita kwenye mashimo au kupita kwenye vitu vigumu ambavyo huwezi kusababisha tairi kupasuka. Ukiona tu uvimbe kwenye tairi yako, basi badilisha haraka.

2. Mtetemeko kwenye matairi
Tairi likianza kutetemeka, basi ni shida inayoweza kutokana na kamba nyembamba za ndani ya tairi kuanza kutawanyika na kujitenga. Ni ngumu kuona tatizo hili kwa macho ya kawaida, bali unaweza kutumia kifaa maalumu wakati wa kufanya msawazisho wa matairi yako (tyres balancing). Unaweza kuhisi hali isiyo ya kawaida kwenye tairi lako, basi unapaswa kubadili au kumuona fundi kwa ushari zaidi.

3. Kuisha kwa kashata (tread)
Kasha ni moja kati ya vitu rahisi sana kujua kuwa sasa unahitaji kubadilisha tairi. Kashata kwenye tairi zina kazi ya kuishikilia gairi kwenye barabara, hivyo basi, kama kashata kwenye gari zimekwisha, gari ina uwezekano mdogo sana wa kutulia barabarani wakati unaendesha, na muda wowote inaweza kukusababishia ajali.

4. Umri wa tairi.
Kila tairi ina chapa ya maelekezo kwenye kifungashio chake. Ununuapo tairi basi soma chapa na itakwambia ni muda gani unatakiwa kutumia tairi hiyo na ni muda gani wa kubadilisha. Ni wazi kifaa chochote kikitumika muda mrefu zaidi, basi hata ubora wake unapungua na kinaweza kisitoe matokeo yanayotarajiwa. Vivyo hivyo kwa tairi, ni lazima ubadili kila muda wake unapokwisha kuepusha ajali zisizo la lazima.

error: Content is protected !!