Onyo latolewa wanaobeba abiria kwenye magari ya mizigo

HomeKimataifa

Onyo latolewa wanaobeba abiria kwenye magari ya mizigo

Wakuu wa usalama barabarani na askari wa kikosi cha usalama barabarani nchini, wameagizwa kutomuonea muhali dereva yeyote wa gari ya mizigo atakayebeba abiria. kamanda mkuu wa kikosi cha usalama barabarani nchini Wilbrod Mutafungwa, alitoa maagizo hayo kufuatia ajali iliotokea katika kijiji cha Mahenge kilichopo wilaya ya Kilolo mkoa wa Iringa ambayo ilihusisha gari la kubeba magazeti.

“Nawaagiza wakuu wa usalama barabarani wa mikoa yote na askari wote wa usalama barabarani kuhakikisha hawamuonei muhari dereva yoyote wa gari la mizigo kuwaachia huru wakabeba abiria. Na magari ya IT, lazima yafuate utaratibu uliowekwa” alisema afande Mutafungwa

Ajali hiyo ilitokea Desemba 13 majira ya saa 10 alfajiri eneo la Lungumba, kata ya Mahenge karibu na mlima Kitonga ikihusisha gari aina ya Hiace lenye namba T 249 DWT, lililokuwa linatumika kubebea magazeti likitokea Dar es Salaam kwenda jijini Mbeya. Kutokana na ajali hiyo watu 10 walifariki na wengine watatu walijeruhiwa huku chanzo cha ajali hiyo kikielezwa kuwa ni mwendokasi uliopelekea gari kumshinda dereva katika kona na kupinduka.

error: Content is protected !!