Wanaotaka kujenga ghorofa kuanzia Jeshi la Zimamoto

HomeKitaifa

Wanaotaka kujenga ghorofa kuanzia Jeshi la Zimamoto

Bunge limefanya marekebisho ya sheria likiweka sharti kwa mtu yeyote anayekusudia kujenga jengo lenye urefu wa kuanzia mita 12 kutoka kwenye usawa wa ardhi (Jengo la takriban ghorofa 3, kuwasilisha mchoro wake wa jengo kwa jeshi la zimamoto kwa ajili ya ukaguzi na ushauri wa kiusalama kuhusu masuala ya moto kabla ya kuanza ujenzi}.

Hayo yamo kwenye muswada wa marekebisho ya sheria ya Jeshi la Zimamoto na uokoaji ambao ulipitishwa juzi na Bunge, na sasa unasubiri kutiwa saini na Rais Samia Suluhu ili uwe sheria kamili.

error: Content is protected !!