Rais Samia: Tanzania imekomaa kidemokrasia

HomeKitaifa

Rais Samia: Tanzania imekomaa kidemokrasia

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania imekomaa na inaongozwa kwa kufuata misingi ya kidemokrasia.

Akizungumza na wanawake waliokusanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku ya demokrasia leo hii, Rais Samia ameeleza namna ambavyo Katiba ya Tanzania imezingatia demokrasia. Amegusia maeneo mbalimbali ikiwemo haki ya kuishi, uhuru wa kujieleza, uhuru wa kukusanyika na maeneo mengi ya haki za binadamu.

“Tunapozungumzia uhuru wa kutoa maoni Tanzania, tumefanya kazi nzuri na tumefanya kazi kubwa. Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa kuwa na vyombo vingi vya habari. Magazeti 257, redio 197, televisheni 50, televisheni mtandao 451, ‘blog’ tunazotazama kwenye simu zetu 122. Na hii ni kwa mujibu wa taarifa ya mwezi Mei 2021. Katika vyombo hivyo vya habari, zaidi ya 75% vinamilikiwa na watu binafsi na kila chombo kinatoa habari zinazoona zinafaa kwa wakati huo. Kwa hiyo uhuru wa kujieleza na uhuru wa habari Tanzania tuko vizuri sana,” amesema Rais Samia.

Hata hivyo, Rais Samia amesema bado kuna changamoto za demokrasia.

“Nchi yetu imekomaa na inaongozwa kwa kufuata misingi ya kidemokrasia. Hata hivyo pamoja na ukweli huo, natambua kuna changamoto za demokrasia bado zipo nchini. Na hii ni kwa sababu kwanza hakuna Taifa duniani ambalo lina ukamilifu katika masuala ya demokrasi. Lakini pili kwa sababu demokrasia pamoja na ukweli kwamba ni lengo au shabaha lakini pia ni mchakato unakwenda hatu moja hadi nyingine,” ameeleza.

error: Content is protected !!