Tetesi za soka ulaya.

HomeMichezo

Tetesi za soka ulaya.

POGBA KUONGEZA MKATABA
KIUNGO wa kati wa Ufaransa, Paul Pogba mwenye umri wa miaka 28, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kujiunga na PSG na Real Madrid, anaelekea kuongeza mkataba katika klabu ya Manchester United baada ya Cristiano Ronaldo kurudi Old Trafford. (Athletic)

BELLINGHAM EURO MIL. 100
KLABU ya Borussia Dortmund ilikuwa inataka euro milioni 100 ili kumruhusu kiungo wake wa kati mwenye umri wa miaka 18, Jude Bellingham kuondoka, huku klabu za Manchester City na Liverpool zikidaiwa kuonyesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo wa England.(Bild)

RICE AWEKEWA BEI
WEST Ham imemwekea bei ya nyota wao, Declan Rice mwenye umri wa miaka 22, ya pauni milioni 100 ili kumuuza kiungo huyo wa England. (football.
london)

MOUNT KUPEWA MKATABA
CHELSEA inajiandaa kumpa mkataba mpya kiungo wa England, Mason Mount hatua ambayo huenda ikamfanya mshahara wake kuongezeka hadi kufikia pauni 150,000 kwa wiki. (90min)

TUANZEBE KUBAKI VILLA
NYOTA wa zamani wa Manchester United na England, Axel Tuanzebe mwenye umri wa miaka 23, anataka kuufanya uhamisho wake wa mkopo katika klabu ya Aston Villa kuwa wa kudumu. (Sun)

BAYERN YAMTAKA WERNER
KLABU ya Bayern Munich inataka kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani na Chelsea, Timo Werner mwenye umri wa miaka 25, katika dirisha la usajili la
Januari. (Football Insider)

LINGARD ATAJWA LEICESTER
LEICESTER City ina nia ya kumsajili kiungo wa Manchester United na England, Jesse Lingard mwenye umri wa miaka 28. (Fichajes)

CHELSEA NA MABEKI INTER
CHELSEA inawanyatia mabeki wa Inter Milan, Alessandro Bastoni mwenye miaka 22 na raia wa Slovakia, Milan Skriniar, 26. (Mediaset)

SPURS YAJITOSA KWA KASSIE
TOTTENHAM Hotspur, imewasilisha ofa ya kumsajili kungo wa kati wa AC Milan, Franck Kessie mwenye umri wa miaka 24, ingawa haijulikani iwapo Spurs
itawasilisha ombi hilo Januari kumsajili nyota huyo wa Ivory (Calciomercato)

GOUIRI AWANIWA LIVERPOOL
LIVERPOOL imeonyesha nia ya kutaka kumsajili straika wa Nice, Amine Gouiri, huku kocha, Jurgen Klopp akionyeshwa kuvutiwa zaidi na nyota huyo wa
Ufaransa mwenye umri wa miaka 21. (Fichajes)

ARSENAL YAMTAKA ISAK
ARSENAL ni moja ya Klabu za Ligi Kuu England zinazomwania straika wa Sweden, Alexander Isak mwenye umri wa miaka 21. (Fichajes via FourFourTwo)

error: Content is protected !!