Ronaldo akaribia kuachana na kibibi cha Turini

HomeMichezo

Ronaldo akaribia kuachana na kibibi cha Turini

Leo Ijumaa Cristiano Ronaldo ametumia saa moja tu katika viwanja vya mazoezi ya klabu ya Juventus kufungasha kilicho chake pamoja na kutoa mkono kwa kwaheri kwa wachezaji wenzake. Kocha Mkuu wa Juventus, Max Allegri amenukuliwa akisema “Ronaldo aliniambia sina mpango wa kubakia Juventus”.

Mechi inayofuata Jeventus itakipiga na Empoli ambapo Ronaldo hatokuwepo kwenye kikosi kitakacho ikabili Empoli siku ya Jumamosi.“Sijavunjika moyo Ronaldo kuondoka, kwani huo ni uamuzi wake binafsi. Tumekuwa nae kwa miaka mitatu, ametoa mchango wake kwa klabu na sasa anataka kuondoka hivyo maisha lazima yaendelee,” amesema kocha Allegri.

Ronaldo aliwasili uwanja wa ndege wa Caselle mishale ya saba mchana na kuondoka na ndege binafsi, huku shauku kubwa ikibaki ni wapi mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 ataangukia. Awali iliripotiwa kuwa Manchester City walitaka kumsajili nyota huyo wa Ureno, lakini tetesi zinaeleza kuwa klabu hiyo imesitisha mpango huo.

Ronaldo alijiunga na Juventus kutoka Real Madrid mwaka 2018 kwa Euro 105 milioni. Akiwa Juventus amefanikiwa kufunga magoli 101 katika ya mechi 134 na kushinda vikombe vitano na miamba hiyo ya Italia. Juventus imedhamiria kumuuza Ronaldo kabla mkataba wake haujakwisha wakati wa kiangazi msimu ujao

error: Content is protected !!