Ferguson atofautiana na Ole kuhusu Ronaldo

HomeMichezo

Ferguson atofautiana na Ole kuhusu Ronaldo

Katika mchezo uliopita wa timu ya Manchester United dhidi ya Everton, wapenzi wengi wa soka walishangazwa na kitendo cha kocha wa timu hiyo, Ole Gunnar Solskjaer kutomjumuisha Christian Ronaldo kwenye kikosi cha kwanza cha timu yake. Miongoni mwa wale ambao walitofautiana na kitendo hicho ni kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson.

Katika video inayomuonesha Ferguson akiwa na bondia Khabib Nurmagomedov ndani ya uwanja wa Old Trafford kama ilivyosambaa jana mtandaoni, Ferguson amesikika akionesha kutokubaliana na kitendo cha Ronaldo kuanzia benchi.

“You should always start with your best player” ni maneno ya Ferguson yaliyomaanisha kwamba “Unapaswa kuanza na mchezaji wako bora”. Kabla ya maneno hayo pia Ferguson amesikika akisema “Nadhani walipoona (Everton) Ronaldo hachezi…” na kuonesha kwamba Everton walipata nguvu baada ya kuona Ronaldo hayupo kwenye kikosi cha kwanza.

Kwa upande wake Ole Gunnar Solskjaer, alitetea uamuzi wake huo kwa kusema kwamba lengo lake ni kuhakikisha anabadilisha kikosi ili kutoa nafasi kwa wachezaji wengi kucheza.

error: Content is protected !!