Rais Samia ameagiza watoto waishio mazingira magumu kusaidiwa

HomeKitaifa

Rais Samia ameagiza watoto waishio mazingira magumu kusaidiwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.Dkt. Dorothy Gwajima kuhakikisha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wanatambuliwa na kusaidiwa.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa usimamiaji wa shughuli za lishe jijini Dodoma, Rais Samia amesema endapo watoto hao watatambuliwa na kusaidia itapunguza wimbi la wahalifu na vitendo vya kiuhalifu kwenye jamii.

“Kuna watoto wanaishi kwenye mazingira magumu na kukua kwao kuna kuwa kugumu kugumu hivyohivyo na hawa ndo panya road wa baadae kwa sababu kama anaishi mazingita hayo magumu ina maana atatoka mapema nyumbani kwenda kujitafutia,

“Hana elimu, hana means (njia) anakwenda kujitafutia kwa means gani (njia)? atakuwa mwizi atakuwa na vitendo viovu alafu tunakuja kupiga kelele panya road tunawazaa wenyewe. Kwahiyo twendeni tukahakikishe Waziri wa Maendeleo ya Jamii hili la kwako, twendeni tukahakikishe watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu tunawatambua na tunawasaidia,” amesisitiza Rais Samia.

 

error: Content is protected !!