Maeneo 7 Tanzania kuonesha fainali za UEFA

HomeMichezo

Maeneo 7 Tanzania kuonesha fainali za UEFA

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amesema mechi ya fainali ya 67 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya(Uefa Champions League Fainal 2022) itakayopigwa Uwanja wa Stade de France nchini Ufaransa Mei 28, mwaka huu, Watanzania watapata fursa ya kushuhudia mtanange huo mubashara katika daraja la Tanzanite jijini Dar es Salaam sambasamba na Filamu ya Royal Tour.

Mchengerwa alifafanua kuwa itaanza kuonyeshwa kwanza Filamu ya Royal Tour iliyomshirikisha Rais Samia Suluhu ambayo imefungua Tanzania duniani, kisha itachezeshwa droo ambapo washindi watatu watakaopatikana watatembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini kwa ufadhili wa Bodi ya Utalii nchini (TTB) na kampuni ya Heineken na mwisho kuonyeshwa mechi hiyo.

Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Heineken ambayo ndiyo mdhamini mkuu wa tukio hilo, Fatma Mnaro amefafanua kuwa lengo la kufanya hivyo ni kutaka kuwafanya wapenzi wa soka walione shindano hilo kwa ubora wa hali ya juu kama ambavyo wtakavyoshuhudia wale ambao watahudhuria mtanange huo jijini Paris, Ufaransa.

Mnaro aliongeza kuwa pamoja na kurushwa mubashara kwenye Daraja la Tanzanite, kuna sehemu mbalimbali za majiji makubwa ambazo pia zitaonyesha ikiwa ni pamoja na The Cask Mwanza, City Pub jijini Mbeya, Arusha, Capetown Fish Market, Samakisamaki na Triple 777 jijini Dar es Salaam.

error: Content is protected !!