Spika Tulia awakingia kifua Mdee na wenzake

HomeKitaifa

Spika Tulia awakingia kifua Mdee na wenzake

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Ackson amesema wanachama 19 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambao walivuliwa uanachama baada ya kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalumu bila kupata baraka ya chama chao bado wataendelea kuwepo bungeni kwani kauli ya mwisho kuhusu wanachama hao inatoka mahakamani.

“Kwa mujibu wa Katiba yetu mamlaka yenye kauli ya mwisho ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mahakama, hivyo katika nchi yenye kuongozwa kwa misingi ya sheria na kuheshimiana kati ya mhimili mmoja mwingine Bunge haliwezi kuingilia mchakato wa mahakama na badala yake inalazimika kusubiri hadi hapo mahakama itakapotoa uamuzi wake kuhusu jambo hilo,” amesema Spika Tulia.

Aidha, Spika Tulia amesema tayari wabunge hao 19 walimtaarifu tangu tarehe 12 Mei mwaka huu kabla hajapokea taarifa rasmi ya uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema kwamba walishakwenda mahakamani kwa ajili ya kulinda haki zao binafsi kama wanachama halali wa Chadema, na wabunge pamoja na kulinda kaiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria ya taifa ya uchaguzi.

Hivyo, kutokana na hayo Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson amesema hawezi kutangaza kuwa nafasi 19 za Wabunge wa Viti Maalum wa CHADEMA ziko wazi, hadi hapo mahakama itakapotoa uamuzi.

error: Content is protected !!