Bob Wine kuhudhuria Baraza Kuu CHADEMA

HomeKitaifa

Bob Wine kuhudhuria Baraza Kuu CHADEMA

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, John Mrema amethibitisha ujio wa aliyekuwa mgombea wa urais wa Uganda kwa tiketi ya chama cha National Unity (NUP), Platform Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine, ambaye anatarajiwa kuwa mgeni maalumu katika kikao cha Baraza Kuu la Chadema litakalofanyika Jumatano Mei 11.

“Bob Wine ambaye ni kiongozi chama kikuu cha upinzani cha NUP cha Uganda atakuwa mgeni wetu mwalikwa maalum katika kikao cha baraza kuu litakalofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City,” amesema Mrema. 

Akizungumza na waandishi wa habari, Mrema aliweka wazi kwamba Baraza hilo linarajia kujadili ajenda tano ambazo ni kipaumbele na mpango mkakati wa chama hicho.

“Katika mpango kazi wa miaka mitano, maana yake tunakwenda kukubaliana namna ya kuvuka kuanzia sasa hadi baada uchaguzi mkuu wa 2025, tunakwenda katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Kwenye mpango mkakati huu tutajadili kwa kina masuala ya Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.

“Baada ya baraza kuu tutawaeleza kile ambacho tumekubaliana katika Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi. Ajenda nyingine itakuwa ni uchaguzi ndani ya chama ambao ratiba yake imekaribia na baraza kuu lina mamlaka kutangaza tarehe rasmi ya kuanza mchakato huu unaonzia ngazi ya chini,” amesema Mrema.

Pia, alieleza kuhusu wanachama 19 ambao walikata rufaa ya kupinga kufukuzwa katika chama hicho mwaka jana 2021.

Miongoni mwa wanachama waliofukuzwa na chama hicho ni Halima Mdee, Ester Bulaya, Agnesta Lambert, Esther Matiko, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga, Tunza Malapo, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Anatropia Theonest, Salome Makamba, Conchesta Rwamlaza na wengineo.

 

error: Content is protected !!