Samia atangaza neema bei ya mafuta nchini

HomeKitaifa

Samia atangaza neema bei ya mafuta nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kwamba kuanzia Juni Mosi mwaka huu Watanzania wataanza kupata unafuu katika bei ya mafuta.

“Nimeamua wananchi waanze kupata nafuu ya bei ya mafuta kuanzia Juni 1, 2022, nimeelekeza serikali tujibane na tujinyime ili kupata fedha kutoka katika matumizi ya kawaida ya serikali ili ziende kutoa nafuu katika bei za mafuta, kwenye kipindi kuelekea mwaka mpya wa fedha,” amesema Rais Samia Suluhu.

Aidha, Rais Samia amesema kesho Jumanne Mei 10, Waziri wa Nishati, January Makamba atatoa maelezo kwa upana zaidi na majibu juu ya suala la upandaji bei wa mafuta kama ambavyo Bunge lilimuelekeza juma lilikopita.

“Nimemwelekeza Waziri wa Nishati aende kufafanua zaidi hatua hii na hatua zingine ambazo serikali inatarajia kuzichukua ili kukabiliana na janga hili, kama Bunge lilivyotaka kesho Waziri wa Nishati atatoa maelezo hayo,” amesema Rais Samia Suluhu.

error: Content is protected !!