Ahadi ya Rais Samia kwa Lissu yatimia

HomeKitaifa

Ahadi ya Rais Samia kwa Lissu yatimia

Rais Samia Suluhu Hassana amekamilisha ahadi yake ya kumsaidia Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu kuweza kupata hati ya kusafiria pamoja na kiinua mgongo chake na malipo ya matibabu.

Akizungumza katika mtandao wa Club House, Lissu alisema alipigiwa simu na mtu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango akamweleza kuwa mafao aliyokuwa akidai yameshalipwa kwa kumaliza madeni aliyokuwa anadaiwa na benki.

“Nilikuwa na madeni ambayo nilikopa katika benki mbili na nilishtakiwa na mojawapo ya benki hizo kwa kushindwa kulipa mkopo uliokuwa unalipwa kupitia mshahara wa ubunge,

“Alivyonipigia simu akaniambia nimelipwa madeni yangu yote kutokana na kiiunua mgongo cha ubunge…kwahiyo naweza nikasema hadharani kwamba (hilo) limeshafanyiwa kazi na ni jambo jema kwa kweli. Sina madeni ya benki na usumbufu niliokuwa nikiupata,” alisema Lissu.

Februari mwaka huu, Lissu alikutana na Rais Samia Suluhu Ubelgiji anakoishi na kufikisha kilio hicho na baadaye alieleza kuwa Mhe. Rais ameahidi kumsaidia.

Lissu alivuliwa ungunge JUni 28 mwaka 2019 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya kutojaza taarifa za mali na madeni na kutotoa taarifa kwa Spika mahali alipo.

error: Content is protected !!