Nyongeza ya 23.3% sio kwa wote

HomeKitaifa

Nyongeza ya 23.3% sio kwa wote

Juzi serikali ilitangaza nyongeza ya asilimia 23.3 kwenye kima cha chini cha mishahara kwa watumishi wa umma, baadhi ya wachumi na wasomi wamechambua ongezeko hilo ambayo italeta ahueni ya ukali wa maisha kwa watumishi na kuongeza mzunguko wa fedha kwenye uchumi.

Kukiwa na matumaini hayo, Profesa Haji Semboja alisema sio kila mtumishi ataongezewa asilimia 23.3.

“Kuna wengine wanalipwa mshahara wa juu, hawa watarekebishiwa kidgo sio kuongezwa kwa asilimia 23.3 haiwezekani,” alisema Profesa Semboja.

Naye Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Tumaini Nyamhokya alisema nyongeza hiyo hupungua kulingana na ukubwa wa mshahara wa mtumishi.

Aidha, alisema wapo watumishi wataoongezewa asilimia chache kwa kuwa wana mishahara mikubwa na inafanyika hivyo ili kulinda uwiano wa mishahara baina ya kima cha chini na mingine.

“Kwa mfano, kima cha chini analipwa Sh300,000 kwa nyongeza hii atalipwa takriban Sh370,000 lakini sio kila kiwango cha mshahara kitaongezewa asilimia hizo,”alisema Tumaini.

Pia alisema nyongeza hiyo itawanufaisha wanaolipwa kima cha chini ambao ndiyo wengi zaidi katika sekta ya umma na kilio kikubwa kilikuwa kwao.

 

error: Content is protected !!