Mambo matatu ya kufanya kujilindaa dhidi ya mhalifu anayefyatua risasi

HomeElimu

Mambo matatu ya kufanya kujilindaa dhidi ya mhalifu anayefyatua risasi

MAMBO MATATU YAKUFANYA KUJILINDA DHIDI YA MHALIFU ANAYEFYATUA RISASI

Katika mazingira ambayo huku yatarajia, aidha benki, barabarani, uwanja wa mpira au kokote pale tukio la mashambulizi ya bunduki/rasasi linaweza kutokea. Matukio kama haya husababisha vifo, hofu na taharuki kwa watu. Sasa je, ni hatua gani za kuchukua kama tahadhari kabla ya tukio, na mambo ya kufanya wakati wa tukio.

1.Kila utakapofika, tafakari namna ya kujiokoa kama kutatokea hatari

Mathalani, ukifika uwanjani kutazama mpira ua tamasha lolote lile, hakikisha kwanza umetambua milango ya dharura. Kwa kuwa ni ngumu kujua ni muda gani tukio baya linaweza kutokea, ni vyema kama utajiuliza maswali kama: Endapo kutatokea shambulizi au hatari, nitafanya nini? Hili haiishii tu katika viwanja vya mpira, bali hata benki, kumbi za sinema, maeneo vya vyuo vikuu, viwanja vya ndege, mgahawani na kadhalika. Kutambua milango ya dharura ni hatua ya kwanza kujihakikishia usalama wako.

Jifunze namna ya kutambua ishara za hatari

Hii inatokana na kusoma majarida, vitabu mbalimbali yanavyochapishwa na taasisi za usalama. Katika dunia ya leo elimu hii imewekwa mtandaoni kwa kujifunza kwa urahisi zaidi. Njia hii itakuhitaji ujifunze zaidi, kujifunza kusoma ishara na alama mbalimbali za watu na mazingira. Mfano, mwendo, mavazi, macho, hata namna ya kuketi, kusimama, sauti, na pia harufu. Hii ni nyanja ya saikolojia ya binadamu, yapo mambo ya msingi ya muhimu kuyajua kwa ajili ya usalama wako na usalama wa wanakuzunguka.

Jitahidi kuondoka eneo hilo mapema

Inawezekana kuna mtu ameanza kufyatua risasi hovyo, ikiwa ni baa, barabarani, kwenye tamasha au kokote kwenye mkusanyiko, kulala chini inaweza kusaidia ikiwa tu mhalifu anapiga risasi katika upande ambao wewe haupo. Lakini hata kama utalala chini, hakikisha haiwi kwa muda mrefu, tazama mazingira ya mhalifu tambaa taratibu na kulala sehemu salama zaidi.Kama ikiwa mhalifu anapiga rasasi upande wako, usilale chini au kuketi chini, ni rahisi sana kwake kukudhuru kwa risasi. Chakufanya ni kukimbia kwa njia ya kupindapinda, ni ngumu risasi kukupata kwa mwendo huo.

Kwa kuwa kabla ya tukio ulipofika eneo husika ulisoma mazingira yako, itakusaidia sana kujua ujisitiri eneo gani ambalo risasi haitokupata. Angalia eneo lenye ukuta au kizuizi kigumu na usimame nyuma yake kupunguza madhara ya risasi.

Kwa kumalizia, kama haupo eneo la tukio, lakini umeona kwenye mitandao kuwa sehemu fulani kuna tukio la mtu kufyatua risasi, usikimbilie kwenye eneo la hatari, kwani unaweza kuhatarisha maisha yako.

error: Content is protected !!