Fanya haya kupunguza gharama za matumizi ya maji nyumbani

HomeElimu

Fanya haya kupunguza gharama za matumizi ya maji nyumbani

Mjadala mkubwa kwa sasa jiji Dar es Salaam ni uhaba wa maji unaopelekea mgao kwenye maeneo mengi.

Tatizo la uhaba wa maji linaweza kutokea mara nyingi kutokana na sababu lukuki, hivyo ni vyema kuchukua hatua za kuweza kupunguza makali ya uhaba huo kwa kupunguza matumizi ya maji.

Zifuatazao ni njia tano zainzaoweza kusaidia katika kupunguza matumizi ya maji;

1. Punguza kiwango cha maji unayotumia kuoga.

Bila shaka kuoga ni kati mambo ambayo hufanya watu watumie maji kila siku. Kwa jiji kama la Dar es Salaam, sio ajabu kuona mtu anaoga mara mbili au hata tatu kwa siku.

Katika kipindi ambacho kuna uhaba wa maji, ni vyema ukaamua kupunguza kiwango cha maji unayotumia kuoga. Kama kwa kawaida unatumia ndoo nzima kuoga, unaweza kupunguza kiwango hicho, lakini pia kama ulikuwa unaoga mara nyingi kwa siku tafuta uwezekano wa kupunguza kiwango hicho.

2. Fanya matengenezo sehemu zinazovuja.

Kuna taarifa nyingi zinazoonesha kwamba kiasi kikubwa cha maji hupotea kutokana na kuvuja kidogo kidogo katika mabomba na sehemu nyingine zinazotumika kuhifadhia maji.

Katika kipindi hiki, unahitaji kila tone la maji hivyo ziba kila sehemu inayoweza kuvujisha maji.

3. Funga bomba wakati unaosha vyombo au kusafisha kinywa

Ni kawaida ya watu wengi kuacha maji yakiwa yanatiririka wakati wa kuosha maji au kusafisha kichwa (kupiga mswaki). Usifanye hivyo, funga bomba na ulifungue pale tu ambapo unakinga maji.

Pia ni muhimu kukinga maji kwenye chombo kama bakuli au sufuria ili uyatumie kuoshea vyombo vingine ili kuepuka hatari ya kutiririsha maji mengi kuliko kiwango halisi unachohitaji.

4. Fanya matumizi mara mbili pale inapowezekana.

Maji unayotumia kufulia au kusuuzia nguo zako, yanweza pia kutumika kufanya usafi wa choo chako na maeneo mengine.

Jitahdidi kfanya hivyo na kuweza pia kutumia maji mara mbili kila inapowezekana.

Jambo lingine la muhimu zaidi katika kipindi hiki ni kuhifadhi maji kwenye vyombo vyote vinavyoweza kuhifadhi maji. Maaji yanapotoka hakikisha unajaza ndoo na vyombo vingine.

error: Content is protected !!