Harmonize atimiza moja ya ndoto zake kubwa

HomeBurudani

Harmonize atimiza moja ya ndoto zake kubwa

Msanii kutoka lebo ya Konde gang Harmonize ameweka wazi kuingia studio na mkongwe wa muziki nchi Tanzania , 20% kutokana na ahadi aliyoweka Oktoba 25, kupitia ukurasa wake wa instagram kwamba kufanya kazi na gwiji huyo ni moja ya ndoto zake hivyo akirudi kutoka Marekani atafanya nae kolabo.

“Going in da studio with my brother 20% asilimia chache sana…!!! Tonight can’t wait,” ameandika Harmonize.

20% ni mshindi wa tuzo tano za Kili Music Awards 2010, aliwahi kutamba na ngoma kama Maisha ya Bongo, Mama Neema, Money Money, Tamaa Mbaya na nyingine kibao amenyoshe yupo tayari na kolabo hiyo kutoka kwa Boss huyo wa Konde Gang.

error: Content is protected !!