Gigy awatolea uvivu Clouds

HomeBurudani

Gigy awatolea uvivu Clouds

Msanii wa kike wa bongo fleva kutoka nchini Tanzania Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amewashukia kituo cha televisheni cha Clouds kwenye ukurasa wao wa Instagram kwakuandika kuwa hajapendezwa na jinsi alivyoandikwa baada ya kutumbuiza usiku wa jana kwenye Uzinduzi wa Chuo rasmi cha Burudani.

“Are you kidding me tambo za who???? Guys embu kubalini yapite na ikiwezekana mumshauri kumlea mwanae, sio mimi please sijapenda caption yenu na kumtag mtu mwingine while sihusiki nae nayeye ajihusishi na mm, naamini ata yeye ajapenda so sitaki ata kama ndio kutafuta attention lakini sio kihivi na sitaki kuhusishwa na maisha ya mtu ambae anisaidii, mimi wala mwanangu please heshimuni maisha ya mtu nimejisikia vibaya like kwanini nimekuja pia sitakiwi kwani yeye sio mwenye clouds basi ilivyo uwezi kumletea kiba story za mond au harmonize na mimi sitaki habari za kima yoyote abegiiii ooo,” ameandika Gigy.

Gigy ameandika hayo baada ya kituo hicho cha televisheni kumuandika kwamba alikua akionyesha tambo zake kwa aliyewahi kuwa mpenzi wake na baba wa mtoto wake Moj360, stejini alivyokuwa anatumbuzi katika uzinduzi wa tamasha la #ExtraUniBash2021.

error: Content is protected !!