Davido agawa fedha zote alizochangisha

HomeKimataifa

Davido agawa fedha zote alizochangisha

Msanii Davido kutoka nchini Nigeria ameamua kuzitoa pesa zote alizokuwa anaomba kutoka kwa marafiki na mashabiki zake kwa ajili ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Davido ametaka pesa hizo ziende kwenye vituo mbalimbali vya watoto yatima nchini Nigeria ambapo jumla ni Naira Milioni 200 huku yeye akiongeza Naira milioni 50 ambazo ni takribani Shilingi za kitanzania bilioni 1 na Nusu.

“Nipende kutoa shukurani zangu za dhati kwa marafiki, ndugu na mashabiki zangu kwa upendo walionionyesha kwakuweza kunisaidia fedha nilizowaomba wanisaidie siku chache zilizopita kwaajili ya kusherekea siku yangu ya kuzaliwa, muitikio ni mkubwa na niliweza kukusanya Naira Milioni 200 ndani ya siku mbili,”

“Nimekua nikipenda kusaidia jamii hivyo basi kiasi cha fedha kilichopatikana Naira milioni 200 nakitoa chote kwaajili ya kusaidia watoto yatima nchini na pia naongeza Naira milioni 50 hivyo kuwa jumla ya Naira milioni 250,” ameandika Davido.

Davido amesema kuwa atakua anafanya hivyo kila mwaka akiwa anasherekea siku yake ya kuzaliwa na kuomba wasanii wenzake na mashabiki kuendelea kumuunga mkono katika kampeni yake hii yakusaidia watoto yatima.

error: Content is protected !!