Tumia asali na maziwa kuondoa sugu

HomeElimu

Tumia asali na maziwa kuondoa sugu

Sugu ni weusi ambao unatengeneza ugumu mara nyingi unatokea katika vifundo au maungio mfano kwenye magoti, nyuma ya vidole vya mikono na nyuma ya kiwiko cha mkono. Sugu zimekua changamoto kwa watu wengi kwani inakufanya uonekane una rangi mbili, utafiti unaonesha ukavu wa ngozi unaweza kusababisha sugu, pia ukavu huo unasababishwa na kutumia kemikali au kutumia sana maji lakini pia sugu zinaweza ksababishwa na magonjwa ya ngozi kama ukurutu na Psoriasis.

Kuna tiba asilia ambazo unaweza kuzitumia nyumbani kwaajili ya kutibu sugu za vidoleni nazo ni kama ifuatavyo;

1. Maji ya limao au ndimu
Limao linatumika kama msaada mkubwa kwenye tiba za nyumbani kutokana na Vitamin C na virutubisho vya antioxidants vilivyopo kwenye limao, Virutubisho vya antioxidants vinasaidia kurejesha afya na kufufua mfumo mzima wa mwili. Jinsi ya kutumia limao kupata matokeo hasi chukua kijiko kimoja cha maji ya limao changanya na sukari, kisha sugua sehemu zenye sugu kwa muda wa dakika kumi kila siku majira ya usiku kabla ya kwenda kulala ukimaliza osha na upake mafuta.

2. Binzari ya Njano asali na Maziwa
Maziwa ni msaada katika urembo kwa kufanya ngozi yako kuwa laini na kuwa kama ya mtoto wapo baadhi ya watu ambao wana hela na wanapenda ngozi zao hutumia maziwa kuogea, ila kwaajili ya kuondoa sugu unatakiwa kuandaa mchanganyiko wa maziwa, binzari ya njano na asali. Chukua binzari ya njano kijiko kimoja kikubwa, asali vijiko vinne vya chakula na maziwa fresh vijiko vinne vya chakula, changanya vitu vyote kwenye chombo kisha paka mchanganyiko huo sehemu zenye sugu na kisha acha kwa muda wa dakika 30 kisha nawa na maji ya uvuguvugu ndani ya siku mbili na utafanya asubuhi na jioni.

3. Mafuta ya Mzeituni na sukari
Mafuta ya mzeituni au Olive oil yana Vitamin A, D, E na K ambavyo vinasaidia kutibu mzio wa ngozi. Andaa mchanganyiko wa mafuta ya zeituni na sukari kwa kuchukua vijiko vikubwa vinne vya mafuta ya mzeiutuni kisha changanya tumia kupaka kama scrub sehemu zenye sugu kwa muda wa dakika 3 mpaka 5 na ukae nayo kwa muda wa dakika 30 kisha nawa kwa maji ya vuguvugu au ya moto fanya hivyo mara mbili kwa siku asubuh na jioni kwa muda wa siku 30.

4. Juisi ya Alovera
Juisi ya Alovera inasaidia kung’arisha ngozi, chukua alovera ondoa lile ganda lake la juu na upake ile juisi yake sehemu zenye sugu na kaa nayo kwa muda wa nusu saa kisha tumia maji ya moto au vuguvugu kujisafisha. Tumia mara mbili kwa siku asubuhi na jioni hadi ngozi yako itakapoanza kung’aa.

error: Content is protected !!