37 waugua na kulazwa kwa kipindupindu Nkasi

HomeKitaifa

37 waugua na kulazwa kwa kipindupindu Nkasi

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Benjamin Chota ameotoa taarifa za kuwepo kwa ugonjwa wa kipindupindu kwani tayari watu 37 ameripotiwa kuugua na kulazwa kutokana na kuibuka kwa ugonjwa huo katika kijiji cha Forodhani, kata ya Korongwe, wilayani Nkasi mkoani Rukwa.

Akizungumza kwenye kikao cha dharura cha kamati ya afya ya msingi Mganga huyo Mkuu alisema taarifa za awali za kuwepo kwa ugonjwa huu ziliripotiwa Desemba 2, mwaka huu na wagonjwa 2 waliripotiwa katika Zahanati ya Korogwe.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijualikali, amewataka wataalamu wa afya kuhakikisha wanachukua hatua zaidi ya kata hiyo na unadhibitiwa uliopoibuka pia aliwaagiza kuhakikisha wanasimamia suala la usafi katika maeneo yote ya wilaya kwa kuwa uchafu na kuwa hatamvumilia mtu ambaye kwa uzembe wake atasababisha ugonjwa huo kusambaa maeneo mengine.

Aidha, alisema sheria za kukabiliana na uchafu zipo kinachotakiwa ni kuzitumia ili kuona mazingira ya kuishi yanakua safi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha maji ya kunywa yanachemshwa au kuwekewa dawa.

error: Content is protected !!