Sababu 3 kwanini usilale na simu kitandani

HomeElimu

Sababu 3 kwanini usilale na simu kitandani

Simu imerahisisha sana maisha ya mwanadamu kwenye nyanja za mawasiliano pamoja na upatikanaji wa taarifa. Hali hii imetufanya tuwe karibu na simu zetu muda mwingi kuliko kawaida, na wengine huenda mbali na kulala nazo kitandani kabisa bila kuchukua tahadhari.

Zipo sababu za msingi za kitafiti na kitabibu ambazo zinakataza tabia za watu kupenda kulala na simu. Na sababu zenyewe ni kama zifuatazo.

1. Inaweza kusababisha moto
Kuna kisa ambacho kilizungumziwa sana miaka ya 2014 ambapo kijana kutoka Texas nchini Marekani, akiwa amelala alianza kuhisi harufu ya kitu kinaungua, aliamua kuinua macho na kutazama kitu gani kinaungua, alikuta simu yake aina ya samsung Galaxy s4 iliyokuwa chini ya mto ikiungua na ilishaanza kuunguza shuka na mto huo. Simu ni kama cha umeme kama ilivyo pasi au mashine ya kusagia matunda, hivyo ni vyema tukajidhari zaidi.

2. Matatizo ya kiafya
Simu inapokua imewashwa inatoa mionzi ili kusaidia upatikani wa mawimbi kwenye simu yako, ikitokea umelala na simu yako basi kutokana na ile mionzi unaweza kupata changamoto za kiafya kama maumivu ya kichwa, maumivu ya misuli, matatizo ya ubongo lakini pia unaweza kupata saratani.

3. Kukosa usingizi
Simu inatoa mwanga wa bluu ambapo kulingana na tafiti, mwanga huo huzuia uzalishaji wa homoni ya melatonin inayochochea usingizi, mwanga huo pia unasabisha macho yetu kuhisi ni mchana jambo linalofanya mtu akose usingizi. Ili upate usingizi mzuri unatakiwa kukaa mbali na simu masaa mawili kabla ya kulala.

error: Content is protected !!