Kwanini Ulaya inanunua mamilioni ya simu mbovu kutoka Afrika?

HomeUncategorized

Kwanini Ulaya inanunua mamilioni ya simu mbovu kutoka Afrika?

Kwa sasa simu milioni 230 zinauzwa barani Afrika, na simu hizi huishia tu kutupwa sehemu zisizo stahili na kusababisha uchafuzi wa mazingira, Kwa mujibu wa mtandao wa E-waste Monitor Afrika,

mwaka 2019 Afrika ilizalisha taka zitokanazo ya teknolojia ya simu tani 2.9. ambapo kati ya hizo ni 1% zilifanikiwa kuhifadhiwa kitaalamu.

Afrika haina teknolojia wala utaalamu wa kuchaka simu na kupata madini madini yaliyomo, hivyo kampuni ya Closing Loop ya Uholanzi na nyinginezo zinanunua simu nyingi sana barani Afrika
na kuzipelekea ulaya kuchenjua madini yaliyomo.

Kila simu ina kiwango cha madini ya thamani kama dhahabu, shaba, platinum pamoja na palladium. Pengine inaweza kukusangaza kuwa simu yako uko nayo kila siku lakin hukuwahi kujua kuwa imeundwa kwa madini ya thamani sana.

> Sababu 3 kwanini usilale na simu kitandani

Tuko katika wakati ambao madini kwenye simu zote yana thamani kubwa kuliko wakati wowote ule, kwani tunaelekea katika wakati ambao tutashindwa kabisa kuchimba tena madini aridhini kutokana na sheria ngumu kimazingira duniani pamoja na kuisha madini aridhini, hivyo simu zetu za mkononi ndizo zitakuwa chanzo kikubwa cha madini.

Simu yako ina madini ya aina gani hasa?

Simu tutumiazo zimeundwa kwa madini ya vito vya thamani. Mathani, iphone ya kawaida ndani yake imeundwa kwa dhahabu gramu 0.03, gramu 0.34 za madini ya fedha, 0.015 gram za madini ya palladium.

Ukiachilia mbali madini maarufu yaliyotajwa hapo juu, simu pia zinayo madini mengine adimu sana ambayo upatikanaji wake aridhini una gharama sana, madini hayo ni yttrium, lanthanum, terbium, neodymium, gadolinium na praseodymium.

Duniani kwa sasa kuna watu zaidi ya bilioni 2 wanaomiliki simu za mkononi na namba hiyo inaarifiwa kuongezeka kwani mali iliyomo kwenye zote hizi ni nyingi zaidi kuliko mgodi wa kawaida, kwani ukiwa na tani 1 iphone inaweza kutoa dhahabu mara 300 zaidi kuliko mgodi wa tani moja wa dhahabu.

Ukiwa na simu milioni 1, unaweza kupata shaba tani 16, fedha (silver) kilo 350, dhahabu kilo 34 na kilo 15 za madini ya palladium.

error: Content is protected !!