Jifunze njia 5 za asili za kujikinga na Malaria

HomeElimu

Jifunze njia 5 za asili za kujikinga na Malaria

Kwa mujibu ripoti ya WHO mwaka 2019, kulikuwa na visa milioni 229 vya Malaria duniani kote. Katika mwaka huo, watu 409,000 walikufa kwa ugonjwa huo hatari.

Watoto chini umri wa miaka mitano wamo katika hatari zaidi ya kuathirika na kufariki kwa ugonjwa huo. Mwaka 2019, katika ya maradhi yote yauwayo watoto, vifo 67% vilisababishwa na Malaria ambapo ni sawa na watoto 274,000 duniani kote.

Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na kimelea kiitwacho Plasmodium, kimelea hiki husambazwa kutoka kwa binadamu mmoja kwenda kwa mwingine na Mbu jike anayejulikana kama Anopheles.

Tumeshatambua kuwa Malaria ni ugonjwa hatari kiasi gani, hivyo basi ni vyema kufuata njia za kitaalamu zinazoshauriwa na wataalamu wa afya kila siku kupitia redio na televisheni. Zipo jitihada nyingine binafsi ambazo tunaweza kuchukua kupunguza usambazwaji wa ugonjwa huu katika mazingira yetu.

Njia hizi ni za asili na hazina na hazina gharama kabisa.

1. Machungwa na Zabibu
Machungwa yana Vitamin C kwa wingi, ambapo yanasaidia kuongeza kinga ya mwili ili kupambana na magonjwa. Zabibu pia zina Vitamin C kwa wingi lakini pia ina kwinini asilia inayosaidia kupamabana na Malaria. Unachotakiwa kufanya ni kutumia juisi ya machungwa au Zabibu iliyotengenezwa nyumbani bila kuongeza sukari. Matumizi ya machungwa na zabibu mara kwa mara huimarisha kinga za miili yetu dhidi ya Malaria.

2. Tangawizi
Tangawizi inaweza kupambana na vidudu lakini pia inaweza kuharibu vimelea vya Plasmodium na kutibu dalili zinazotokana na malaria kama maumivu kichefuchefu, kutapika na kukosa hamu ya kula. Matumizi yake ni kutafuna tangawizi kila siku au unaweza kuchagua kunywa chai ya tangawizi mara mbili kwa siku.

Jinsi ya kutengeneza chukua tangawizi isugue kwenye chombo na weka vikombe viwili vya maji kisha chemsha ikishachemka epua na uiache ipoe, ikishapoa unaweza kuichuja tayari kwa kunywa unaweza kuongezea asali na maji ya limao.

> Baada ya miaka 10, chanjo ya kwanza ya Malaria yathibitishwa

> Maajabu: Ujio wa Mbu vipofu wasioona binadamu

3. Mchaichai
Mchaichai ni maarufu zaidi na wengi na tunautumia kama kiungo kwenye chai kuongeza ladha. Unatakiwa kuchukua majani ya mchaichai kisha uchemshe na kisha unywe kila siku. Unywaji wa maji yenye mchaichai unaimarisha kinga ya mwili dhidi ya maradhi mbalimbali ikiwemo Malaria.

4. Kabila mazalia ya Mbu
Usiruhusu katika mazingira unayoishi kuwepo na mazingira rafiki yanayoweza kustawisha uzalianaji wa Mbu. Mbu hupendelea kutaga mayai kwenye madimbwi ya maji, sehemu zenye unyevunyevu na hata vichaka.

Mazingira haya siyo rafiki kwako, unapaswa kuziba kwa vifusi madibwi kuondo utagwaji wa mayai ya Mbu, punguza vichaka, matawi na nyasi katika mazingira yako, piga dawa za kuulia mazalia ya Mbu na kisha lala ndani ya neti yenye dawa. Hapo utafanikiwa kupambana na Malaria.

5. Apple Cider Vinegar (Vinega ya Tufaa)
Hii ni dawa ya zamani inayotumika kutibu homa na kupunguza joto la mwili lakini pia huimarisha mfumo wa kinga na kusaidia mwili kupona haraka kutokana na magonjwa. Unachotakiwa kufanya ni kutumia kila siku hadi upate nafuu kabisa.

Tumia vijiko viwili vya Apple Cider Vinegar na changanya na maji safi kiasi cha chupa ndongo ya lita moja kisha kunywa. Fanya hivyo mara mbili.

Jinsi ya kuandaa ongeza vijiko viwili vya Apple Cider Vinegar kwenye glasi ya maji safi na unywe hii inapaswa kufanyika mara mbili kwa siku.

error: Content is protected !!