Ini Edo awajia juu wanaohoji kuhusu mtoto wake

HomeBurudani

Ini Edo awajia juu wanaohoji kuhusu mtoto wake

Mwigizaji wa Nollywood, Ini Edo amejibu watu wanaosema kwamba mtoto wake amempata kwa bahati kutoka kwa mfadhili aliyetoa mbegu zake na kuunganisha na za mrembo huyo kama njia moja wapo ya kuweza kupata mtoto na sio njia za kawaida zinazojulikana.

“Mfadhili wa binti yangu sio mtu wa kubahatisha. Msimfanye zaidi ya kuwa mtoaji tu basi na sasa mnaweza kuendelea na maisha yenu mniache na mimi,” aliandika Ini.

Alipoulizwa kwanini amechagua njia hii kupata mtoto na sio kama ilivyozoeleka kwamba mwanamke abebe mimba ndio ajifungue na kupata mtoto, yeye alisema amechoka kuona malumbano kati ya baba na mama hivyo asingependa mwanae apitie changamoto hiyo.

“Nilichagua njia hii ya kupata mfadhili kwa ajili yangu na amani ya mtoto wangu. Sababu nyingine kubwa ni kwamba inanipa shida sana nikiona malumbano kati ya baba na mama juu ya mtoto kwenye vikao na pia mtoto kuchukuliwa na kwenda upande mmoja kukiwa na matatizo,” alisema Ini Edo.

error: Content is protected !!