Davido amuomba hela Diamond Platnumz

HomeKimataifa

Davido amuomba hela Diamond Platnumz

Msanii Davido kutoka nchini Nigeria, akiwa kwenye maandalizi ya siku yake ya kuzaliwa amekuja na staili mpya ya kuomba hela watu wake wa karibu kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo amewataja baadhi wa wasanii na kuwaambia wamtumie fedha huku mmoja wapo akiwa ni Diamond Platnumz kutoka Tanzania.

Davido ameweka nambari za akaunti yake ya benki ambayo anasisitiza wasanii wamtumie hela kisha kurekodi video huku akiwataja wasanii mbalimbali kutumia namba hizo, baadhi ya wasanii aliowataja ni Focalistic kutoka Afrika Kusini, Stanley Enow kutokea Cameroon, Tiwa Savage, Zlatan , Mayorkun, Mr Eazi na wengine wengi.

Mpaka sasa wasanii waliomtumia ni Zlatan, Adenkule, na Teni huku wengine wakiendelea kutuma, Davido anasherehekea siku yake ya kuzaliwa kila tarehe 21 Novembana mpaka sasa ameshakusanya jumla ya Naira milioni 33 sawa na shilingi milioni 184, 920, 264, 47/- za kitanzania.

error: Content is protected !!