Machinga wadaiwa kuvamia Kanisa

HomeKitaifa

Machinga wadaiwa kuvamia Kanisa

Kanisa la Orthodox, Jimbo la Dar es Salaam, limedai kwamba wafanyabiashara ndogo (machinga) wamevamia eneo la Kanisa lao lilipo mtaa wa Salasala katika wilaya Kinondoni, baada ya kuondolewa katika maeneo yasiyokuwa rasmi.

Makamu Askofu wa Kanisa hilo Jimbo la Dar es Salaam, Cleophace Bachuba ameiomba Serikali kuwaondoa wafanyabiashara waliojenga vibanda kwenye eneo hilo kwani wamekuwa wakiwafanya washindwe kushiriki vyema ibada.

Naye Paroko wa Kanisa hilo, Padri Frumentosi Msuri amesema “Tumeshajenga ukuta upande wa mbele ya Kanisa, bado upande wa kulia ambako sasa ndiko wamejazana, hata ukitaka kuingia na gari huwezi kuingia”

>Hii ndiyo mitaa 4 iliyotengwa kwa Machinga wa Kariakoo

Hata hivyo, wakati Kanisa likisema eneo hilo ni la kwao tangu mwaka 1993 walipopatiwa na muumini wao, Serikali katika mtaa wa Salasala imesema eneo walilopo wamachinga hao sio la Kanisa.

Mwenyekiti wa mtaa huo, Robert Massawe amesema wafanyabiashara hao wameruhusiwa kufanya biashara zao katika eneo hilo la wazi lililopo pembeni ya  Kanisa. Amesema wanakamilisha ujenzi wa vyoo katika eneo la Kisanga, ili wamachinga hao wakapangwe rasmi katika eneo hilo.

Nye Mwenyekiti wa Wamachinga hao, Kizito Ponsiano amesema eneo hilo ni la wazi, lakini amewaomba viongozi wa Kanisa kuleta vielelezo vinavyoonesha kwamba eneo hilo ni la Kanisa, akisistiza kwamba iwapo watapewa vielelezo hivyo na kujiridhisha, wataondoka katika eneo hilo.

 

error: Content is protected !!