Eric ten Hag kuinoa Man U

HomeMichezo

Eric ten Hag kuinoa Man U

Klabu ya mpira ya Uingereza, Manchester United imefikia makubaliano na Erik ten Hag kuwa meneja wao wa kudumu mapema leo Aprili 13, 2022.

Makubaliano hayo ya mdomo yatafuatiwa na mkataba wa miaka minne kati ya ten Hag na Man U.

Ajax, ambapo kwa sasa bado ten Hag anafanya nao kazi wanafahamu hali ilivyo kwa sasa na bado hawajafikia makubaliano na Man U. Kwa sasa hakutakuwa na makabidhiano ya mkataba wala matangazo rasmi hadi mchezo kati ya Ajax na PSV Eindhoven katika fainali ya Kombe la Uholanzi utakapokamilika Aprili 17.

Ten Hag atachukua nafasi ya Ralf Rangnick, ambaye amekuwa akifanya kazi hiyo kwa muda tangu meneja wa zamani wa timu hiyo, Ole Gunnar Solskjaer kutimuliwa kazi na klabu hiyo ya Ligi ya Premia mwezi Novemba.

error: Content is protected !!