Fahamu mambo 50 kuhusu Mwl. Nyerere

HomeElimu

Fahamu mambo 50 kuhusu Mwl. Nyerere

Leo ikiwa ni kumbukizi ya miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Baba wa Taifa) na Rais wa Kwanza wa Tanzania. Haya hapa ni baadhi ya mambo yanayomuelezea Mwalimu Nyerere.

  1. Jina alilopewa na wazazi wake ni Kambarage Nyerere.
  2. Alipewa jina Julius akiwa na miaka 20 baada ya kubatizwa mwaka 1942.
  3. Alisaidia kuipatia Tanganyika uhuru Desemba 9, 1961.
  4. Aliasisi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
  5. Nyumba aliyoishi Magomeni akipigania uhuru hivi sasa ni sehemu ya makumbusho ya kitaifa.
  6. Alileta Ujamaa na kujitegemea.
  7. Alishiriki kwenye shughuli za ukombozi wa Afrika.
  8. Alipigania uhuru wa vyombo vya habari hata vile vya nchi nyingine za Afrika.
  9. Alipenda kuudumisha tamaduni wa Watanzania.
  10. Kutokukubali kulewa madaraka.
  11. Mwalimu hakuwa anajua kuendesha gari.
  12. Alikuwa anavuta sigara (clipper) paketi mbili kwa siku hadi mwaka 1962 baada ya kifo cha rafiki yake Hamza Mwapachu.
  13. Alifunga ndoa na Mama Maria Nyerere mwaka 1953.
  14. Alisoma Astashahada ya ualimu Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda 1943 -1947.
  15. Aliingia Makerere akiwa na miaka 20.
  16. Kwa mara ya kwanza kuvaa viatu alikuwa na miaka 20.
  17. Mwalimu Nyerere alikuwa mtoto wa Chifu Nyerere Burito wa Zanaki.
  18. Baba wa Mwalimu Aliitwa Nyerere “Nzige” kwa kilugha kutokana na kuzaliwa kipindi ambacho kulikuwa na uvamizi wa nzige kijijini hapo.
  19. Burito alikuwa na wake 22 na watoto 25.
  20. Mama wa Mwalimu Nyerere alikuwa mke wa tano wa Chifu Burito, Mwalimu akiwa ni mtoto wa pili kati ya nane wa mama huyo.
  21. Alisoma Tabora Boys.
  22. Alitetea haki za wanawake.
  23. Alikemea mila kandamizi.
  24. Alikemea sana rushwa.
  25. Kabla ya kuwa Rais wa kwanza alikuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika mwaka 1961 -1964.
  26. Hakupenda uchu wa madaraka.
  27. Alikuwa mwalimu huko Pugu kabla ya kuwa Rais hivyo akabaki na jina la Mwalimu Nyerere.
  28. Alizaliwa Aprili 13, 1922.
  29. Alianza shule akiwa na miaka 12.
  30. Alibatizwa na kuwa Mkatoliki akiwa na miaka 20.
  31. Alikuwa Mtanzania wa Kwanza kusoma Chuo Kikuu cha Edinburg, Uingereza na kupata Stashahada ya Uzamili 1949 -1952 .
  32. Mwaka 1953 alikuwa Rais wa Tanganyika African Association (TAA).
  33. Mwaka 1954 alibadili TAA na kuwa Tanganyika African National Union (TANU).
  34. 1958 aliingia kwenye Bunge la wakoloni.
  35. Alikuwa sehemu ya upatanishaji wa vita ya Burundi 1996.
  36. Oktoba 14, 1999 alifariki huko London kutokana na saratani ya damu.
  37. Alipenda sana kucheza bao.
  38. Aliwahi kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  39. Aliasisi usawa wa kijinsia.
  40. Ameondoa ukabila.
  41. Hakuupa nafasi ubaguzi wa rangi.
  42. Aliamini katika maendeleo ya elimu ili kuondoa ujinga, umaskini na maradhi.
  43. Alikikweza kilimo kama uti wa mgongo wa nchi.
  44. Alishiriki kudumisha amani na umoja ndani ya Tanzania.
  45. Alileta ushirikiano wa kitaifa.
  46. Alianzisha ushirikiano wa kimataifa.
  47. Aliruhusu uhuru wa kuabudu kadiri ya imani yako.
  48. Alikuwa miongoni mwa waasisi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  49. Aliasisi Azimio la Arusha .
  50. Alikuwa Mwenyekiti wa CCM hadi kufikia mwaka 1990.
error: Content is protected !!