Agizo la Dkt. Mpango kwa Nape

HomeKitaifa

Agizo la Dkt. Mpango kwa Nape

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amemuagiza Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata habari zote kuhusu Maadhimisho ya Miaka 58 ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza wakati maadhimisho hayo yakiendelea jijini Dodoma, Dkt. Mpango amemtaka Waziri Nape kuhakikisha hafla ya leo inarudiwa mara kadhaa kwa manufaa ya wale waliokosa kuangalia siku ya leo.

“Sijamuona Waziri wa Habari [Nape Nnauye] humu ndani, lakini popote alipo bila shaka atanisikia… ninamtaka Waziri wa Habari, arushe tukio hili mara kwa mara kwenye vyombo vyetu vya habari. Nawashukuru kwa kulirusha tukio hili mbashara lakini mrudierudie ili wale ambao hawakupat uhondo huu waweze kupata fursa hiyo na elimu kubwa.

Aidha, amewakumbusha wananchi umuhimu wa sensa ya watu na anuani za makazi.

error: Content is protected !!