Zitto Kabwe afunguka sakata ya kuachiwa kwa Mbowe

HomeKitaifa

Zitto Kabwe afunguka sakata ya kuachiwa kwa Mbowe

Hadi kufikia mwaka 2015, Tanzania ilikuwa katika hatua nzuri ya kuelekeza ukomavu wa demokrasia ya vyama vingi. Licha ya watu wengi kuonekana kuunga mkono harakati za demokrasia ya vyama vingi, bahati mbaya harakati hizo zilipatwa na vikwazo vingi sana na hatimaye demokrasia kuanza kusuasua.

Tangu mnamo mwaka 1992 demokrasia ya vyama vingi ilipoanzishwa nchini mwetu, imani ya watu juu ya demokrasia ya vyama vingi nchini Tanzania imekua ikiongezeka kila uchwao ukilinganisha na aina nyingine za mifumo ya kiutawala wa nchini.

Kamisheni ya Nyalali ilipotoa ripoti yake mwaka 1991, ilionesha kuwa ni watanzania 20% ndio walionesha kuwa na imani ya demokrasia ya vyama vingi, mwaka 1994 utafiti wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ulionesha kuwa ni 36% pekee ya watanzania ndio wana imani ya mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Namba ya watu kuwa na imani ya demokrasia ya vyama vingi iliongezeka zaid mwaka 1991 kwenye utafiti uliofanywa na Bernadetta Killian, ambapo ilioneonekana kwamba asilimia 77% ya watanzania wana imani na mfumo wa demokrasia ya vyama vingi.

Licha ya kuwa na idadi kubwa ya watu wanao unga mkono demokrasia ya vyama vingi, lakini uhalisia wa takwimu huo haupo kwenye maisha ya kweli, isipokuwa umo kwenye makaratasi tu, hasa hali mbaya ya demokrasia nchini mwetu inaweza kudhihiri kati ya kipindi cha 2015 – 2020 ambapo hakukuwa na uhuru kabisa wa kufanya shughuli za kisiasa kama vile mikutano ya hadhara, kubanwa na kufungwa kwa vyombo vya habari na mbaya zaidi kupiga ngwala uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 pamoja na Uchaguzi Mkuu 2020.

Bila shaka hali ya sasa ya demokrasia ya Tanzania haina tofauti na ile ya 1992 ambapo mabunge yote ya Tanzania bara na Zanzibar walitawaliwa na chama tawala, CCM, ambapo kila Bunge CCM ilikuwa na wawakilishi kwa asilimia 97%. Polisi bado wanatekeleza dhuluma, kuzuia mikutano halali ya hadhara, kutesa viongozi wa upinzani na kadhia nyinginezo, na huku Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA Freeman Mbowe akiendelea kusalia korokoroni kwa makosa ya ugaidi ambao tunaamini ya kubambikiwa.

Hata hivyo, maombi ya Katiba Mpya hayana muafaka, na mchakato na kelele za kupata tume uhuru ya uchaguzi bado ni kizungumkuti kwani chama tawala kimekubali kuwa masito juu ya hilo.

Mengi yaliyotangulizwa kutajwa hapo juu yamefanywa wakati wa utawala na hayati John Pombe Magufuli alifariki Dunia Machi 17, 2021. Rais Mpya, Samia Suluhu Hassan aliyatwaa madaraka kutoka kwa mtangulizi wake na kuja na tumaini jipya kwa watanzani, bahati mbaya maneno yake hayakudumu. Miezi mitatu baada ya kuingia madarakani, wimbi la kuzuia mikutano ya hadhara ya siasa iliendelea kupigwa kufuli kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake.

Uongozi wa TCD (Tanzania Centre for Democracy)

TCD ni jukwaa la mijadala linalohusisha hasa vyama vya siasa vywenye uwakilishi Bungeni. Chama cha ACT kilishiriki mjadala ulioandaliwa na Jeshi la Polisi kujadili namna ya kuondoa migongano na mikwaruzano na vyama vya siasa. Vyama vingine kama NCCR – Mageuzi pamoja na CHADEMA kivikataa kushiriki mkutano na Polisi kwa madai kwamba Jeshi la Polis sio watunga sera, hivyo wangeomba Waziri mwenye dhamana juu ya Jeshi la Polisi aandae mkutano huo na si Jeshi la Polisi. Nilichukua uamuzi wa kuadika barua kwa Waziri Mkuu Kassim majaliwa kumuomba mawaziri wawepo kwenye mkutano huo na ombi langu likakubaliwa.

Barua niliyoituma kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa nilimhusisha na Msajili wa Vyama vya Siasa Francis Mutungi, ambaye aliweza kuandaa kikao Octoba 22 -23 2021 ambapo kikao hicho, tarehe yake iligongana na tarehe ya TCD iliyotangazwa maoema na bahati mbaya vikao vyote kutofanyika, cha TCD pamoja na kile cha msajili wa vyama vya siasa.

Tarehe mpya ya mkutano ikapangwa, na wakati huu Rais wa Samia alibariki ufunguzi wa mkutano huu jijini Dodoma kujadili hali na mustakabali wa demokrasia nchini mwetu. MKutano ule ulifanyika kwa siku mbili, kuanzia Disemba 15 – 17 2021. Msajili wa Vyama vya Siasa aliweza kualika wawakilishi kutoka makundi mbalimbali kama vile asasi za kiraia, viongozi wa dini mbalimbali na watu mbalimbali wenye ushawishi nchini.

Mkutano wa TCD uliotajwa awali, umeghairishwa na umepangwa kufanyika Februari 2022, imekubaliwa kwamba mkutano wetu wa Februari utajadili hasa masuala ya mkutano wa vyama vya siasa uliofanyika Dodoma.

Kwanini ACT – Wazalendo ilishiriki Mkutano wa Dodoma?

Baada ya mkutano wa ndani Chama cha ACT kwa dhati kabisa tulikubaliana tushiriki mkutano wa Dodoma kwa lengo la kufanya majadiliano juu ya hali ya kidemokrasia pamoja kutafuta mwafaka. Nukuu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ilitupa mwangaza wa dhamira yetu, “Mlango Ukifungwa, jitihada za kuufungua lazima zichukuliwe, kama umesikindikwa, basi ulazimshwe hadi ufunguke wote, Kwa hali yoyote ile mlango haupaswi kulipuliwa, kwa maslahi ya walio ndani”..

Nafasi angalau ya kufanya majadiliano na Serikali juu ya hali ya kidemokrasia nchini ni ishara ya mlango kusindikwa (Upenyo), ACT tukajitahidi kuusukuma na kuingia ndani tukiwa na ajenda zetu mahususi. Binafsi niliongoza ajenda ya chama chetu kwenye mjadala wa Dodoma, pia Kaimu Mwenyekiti wa chama chetu Bi. Dorothy Semu, Katibu Mkuu Ado Shaibu, Mwenyekiti wa Bodi yetu wa Wadhamini Bi. Mhonga Ruhwanya, na Mwanasheria wetu, ambaye pia ni Waziri wa Biashara Zanzibar, Omar Said Shaabani.

ACT tulikuwa na ajenda kuu nne

1: Kwanza kikwazo cha kufanya mikutano ya vyama vya siasa kiondolewe, pia kifungu cha sheria cha 258 sheria ya vyama vya siasa zibadilishwe ili kuboresha mazingira ya vyama vya siasa nchini

2: Sheria ya Uchaguzi kifungu cha 343 kifungwe kifutwe, hii itawezesha kuwa na tume huru ya uchaguzi na kusaidia Uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu

3. Mchakato wa kuwa na Katiba Mpya uliositiswa, uendelee

4. Mwenyekiti wa CHADEMA aachiwe huru bila masharti yoyote ili kutoa mwanya kuendelea kuliponya taifa.

Mbowe Kuachiwa

Ndani ya siku mbili za majadiliano, nikiwa kama Mwenyekiti wa TCD nilipewa nafasi ya kuzungumza machache mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan. Nilitumia fursa hii adhimu kuzungumzia hasa ajenda yetu namba nne, nilizungumza kwa utii mkubwa kuepuka kuonesha kwamba naishinikiza na kuidharau serikali. Nilimuasa Rais Samia atumie njia za sheria kuhakikisha kwamba mashitaka dhidi ya Mbowe yanaondolewa, Rais Samia alijibu kuonesha kuna uwezekano wa Mbowe kupewa msamaha. Hatua ya mimi kuzungumza juu ya Mbowe mbele ya Rais ilizua mtafaruku mkubwa kwangu kutoka kwa wafuasi wa CHADEMA, wakidai kile hata mimi ninachoamini kwamba, Mbowe hana hatia.

Binafsi naamini kesi ya Mbowe ni kesi ya kisiasa, basi hata muafaka wake unaweza kupatikana kisiasa. Nilifika kumtembelea Mbowe gerezani siku ya maandisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania, na nilipata ridhaa yake juu ya suala la kuzungumzia kesi yake. Nilipomtembelea niliweza kumpatia na vitabu kadhaa.

Cheche na makali kutoka kwa wafuasi wa CHADEMA yavikunizuzua kwani tayari nilishapata ridhaa kutoka kwa mhusika mkuu ambaye ni Mbowe. Nasema kwa yakini kabisa, Mbowe hakuhitaji msamaha, na wala binafsi sikutamka kumuombea msamaha, mzozo juu ya jambo hili, ni suala na utata kwenye ufikishaji wa taarifa, jambo ambalo sina udhibiti nalo.

Katika hotuba yake, Rais Samia alisema kwamba, “Mikutano ya kisiasa ni haki ya vyama vya siasa”, lakini hakutoa tamko lolote kuhusu kulifungulia, Rais Samia kinyume chake akaishia kuhimiza vyama vya siasa ziunde mikakati ya kujithmini. Mkutano wa Dodoma ulijadili kwa kina jambo hili, na mapendekezo mengi yametumwa kwa Rais Samia kueleza dhamira ya vya siasa kupinga mikuano ya hadhara, na inaonekana Rais Samia kukubali kuondoa zuio la vyama vya siasa kufanya mikutano endapo tu vyama vya siasa vitakuja na mkakati wa kujitathmini.

Ukweli na Uwazi kwenye mjadala

Mkutano wa wadau wa vyama vya siasa jijini Dodoma ulifanyika kwa uwazi zaidi, wadau wa vyama vya siasa na demokrasia walizungumza zaidi juu mkatako wa Uchaguzi Mkuu wa 2019 – 2020 ambao ulionekana dhahiri kuwa batili ambao vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu vilitamalaki kote Tanzania Bara na Zanzibar. Pia Mkutano uligusia polisi kubughudhi upinzani bila sababu za msingi na pia kugusia suala la mchakato wa Katiba uliokwama.

Kulikuwa na makubaliano na wito kutoka kwa washiriki kuendea hatua ya kuliponya taifa majeraha makubwa yaliyotokana na uongozi uliopita, na lazima serikali ikubali kwamba ilifanya makosa na kufungua ukurasa mpya kujenga Demokrasia. Nukuu kutoka kwa Rais, “Ni kweli kuna vidonda, malamiko na maumivu”.. ilituongoza kwenye mkutano wetu, kujenga imani miongoni mwetu na kuendelea mbele katika namna ya kuboresha demokrasia nchini mwetu.

Mizengo Pinda, Waziri Mkuu mstaafu na mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM, alisema kwamba ni lazima serikali isikilize matakwa ya kuwa na tume huru ya uchaguzi. Alisema, “Huwa napata aibu sana, kuona CCM inatangazwa mshindi kwa 90% ya kura zote nchini, sote tunajua kuwa haiwezekanI” Maridhiano yamefikiwa kwenye baadhi ya mambo, bado kazi kubwa inapaswa kufanywa kumalizana na yale ambayo hayajapata muafaka.

Maazimio yaliyofikiwa Dodoma

Siku ya tatu ilianza na Jaji Mstaafu Joseph Warioba, aliyekuwa Waziri Mkuu, akitoa majumuisho ya mambo muhimu ambayo hayakuwa na mabishano kutoka kwa washiriki na kuuendesha mkutano huo ili kujenga muafaka juu ya swali la Katiba. Masuala manne yalikuwa na uthibitisho wa wazi kutoka kwa washiriki (Maazimio ya Dodoma):

Mbili, kwamba Tume Huru ya Uchaguzi lazima iundwe chini ya sheria mpya ya uchaguzi. Ilikubalika kuwa mchakato wa kuandaa muswada huo lazima uanze mara moja.

Tatu, kwamba mchakato wa kuunda Katiba Mpya ukamilike, ingawa ni mara moja tu sheria mpya ya uchaguzi itakapowekwa. Hii ni ili tume huru ya uchaguzi isimamie mchakato wa kura ya maoni ya katiba.

Na, nne, mikutano ya hadhara inapaswa kufurahishwa na vyama vya siasa kwa mujibu wa sheria pindi kanuni za kujiendesha zitakapowekwa.

Kwa jumla, masuala 80 yaliibuliwa katika majadiliano ya siku tatu na Kikosi Kazi kiliundwa kitakachosimamia ufuatiliaji wa utekelezaji wa masuala yaliyoibuliwa na kukubaliana kuhusu muda wa utekelezaji.

Kama mdau wa siasa, ninayachukulia Maazimio ya Dodoma kama sehemu ya kuanzia kuelekea mjadala wa kisiasa unaojumuisha zaidi nchini. Maazimio haya yanajumuisha masuala muhimu ya wasiwasi yaliyotolewa na wanaharakati wa kisiasa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Hatua zinazofuata zinaweza kuwa ngumu zaidi lakini ikiwa wahusika wote wa kisiasa na washikadau wakuu watahusishwa vikwazo vinaweza kuondolewa.

Katika utekelezaji wa yale yaliyokubaliwa, ni muhimu wahusika wakuu ambao hawakushiriki Mkutano wa Dodoma wafikiwe na kushawishika kuhusika. Baadhi ya wanaogomea wanaweza kudai makubaliano ikiwa ni pamoja na tetesi na Mkuu wa Nchi, naomba ikubaliwe.

Suluhu ni mchakato

Tanzania imepitia kuzimu katika miaka mitano iliyopita. Mtu akiandika historia yetu na mgeni akasoma sura kuhusu miaka mitano iliyopita, hawezi kuamini kuwa anasoma kuhusu Tanzania.

Ikiwa fursa zinazotolewa na Mpango wa Dodoma hazitachukuliwa, mvutano utaendelea na kuweka mazingira wezeshi kwa marudio ya miaka mitano iliyopita. Nimejifunza kutoka kwa watani wa chama changu kutoka Zanzibar kwamba maridhiano ni mchakato, si tukio.

Maazimio ya Dodoma ni hatua katika mwelekeo sahihi kwa Tanzania kurejea katika njia yake ya kidemokrasia. Ni muhimu nimalizie makala hii kwa kusisitiza kwamba si lazima sote tukubaliane kwa kila jambo.

Levitsky na Ziblatt wanavyoandika katika kazi zao za kina, How Democracies Die, kuhusu miungano ya kutetea demokrasia, “Miungano ya watu wenye nia moja ni muhimu, lakini haitoshi kutetea demokrasia. Miungano yenye ufanisi zaidi ni ile inayoleta pamoja makundi yenye mitazamo tofauti – hata ya kupingana – juu ya masuala mengi.”

Mlango umefunguliwa, tuijenge upya demokrasia yetu

Hii ni tafasiri ya andiko halisi lililoandikwa kwa lugha ya kingereza na Mh. Zitto Kambwe kupitia tovuti ya The Chanzo

error: Content is protected !!