Ndugulile atoa neno la mwisho, akabidhi ofisi

HomeKitaifa

Ndugulile atoa neno la mwisho, akabidhi ofisi

Aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amekabidhi ofisi kwa waziri mpya, Dkt. Ashatu Kijaji na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumpa fursa ya kuhudumu katika wizara hiyo katika kipindi cha miezi sita.

Dkt. Ndugulile ambaye ni Mbunge wa Kigamboni amewataka watendaji wa wizara hiyo kuendeleza mazuri yaliyofanyika na kwa nguvu ile ile waendelee kutekeleza mazuri mengi zaidi kwa kushirikiana kwa karibu na Dkt. Kijaji kwa kuwa anaondoka katika wizara hiyo akiwa ameiacha katika mikono salama.

Kwa upande wake Dkt. Kijaji amemtaka Dkt. Ndugulile asifunge milango kwa sababu bado ni mdau mkubwa katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya nchi kupitia utendaji wa Wizara hiyo mtambuka na wezeshi kwa Wizara na taasisi za Serikali katika kuongeza ufanisi, uwazi na uwajibikaji wa pamoja kupitia huduma za mawasiliano na TEHAMA.

“Sisi wote ni watanzania lengo letu ni kuijenga Tanzania hivyo uzalendo wetu, upendo wetu pasipo chuki na umoja wetu ndio kitakachofanikisha kutimiza malengo tuliyojiwekea,” amezungumza Dkt. Kijaji.

error: Content is protected !!