Mkakati wa NIDA, TRA na Bodi ya Mikopo kusaka wadaiwa

HomeKitaifa

Mkakati wa NIDA, TRA na Bodi ya Mikopo kusaka wadaiwa

Serikali imeendelea kutoa mikopo kufadhili masomo ya elimu ya juu kwa wanafunzi nchini ambapo inategemea kutumia Tanzania shilingi bilioni 570 kwa mwaka huu wa fedha.

Lakini pia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania (HESLB) kupitia afisa uhusiano wa umma amewakumbusha wadaiwa wote kuendelea kulipa madeni yao na kuachana na tabia ya kutolipa madeni hayo kwani hivi sasa bodi inashirikiana na taasisi zote za serikali na zisiso za serikali kuhakikisha wadai wote wanalipa.

Katika mkakati huo, inatarajia kushirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwapata wadaiwa wote.

error: Content is protected !!