Bei za mafuta duniani zimepanda hali ambayo imethiri pia bei za mafuta ha Tanzania. Tumekuwekea sababu 5 zinazoweza kupelekea kupanda kwa bei hizo duniani:
1. Ushawishi wa OPEC
OPEC ni jumuiya ya nchi zinazosafirisha mafuta (Organization of Petroleum Exporting Countries). Kwa sasa jumuiya hiyo inaundwa na nchi 13: Algeria, Angola, Congo, Guinea ya Ikweta, Gabon, Iran, Iraq, Kuwait, Libya, Nigeria, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Venezuela.
Kwa mujibu wa takwimu za OPEC hadi kufikia mwaka 2018, nchi za OPEC zinasambaza tarkibani 80% ya mafuta yanayotumika ulimwenguni. Jumuiya hiyo ina nguvu kubwa katika kuamua kushuka au kupanda kwa bei za mafuta duniani. Mfano, mwaka 2014, OPEC ilisema itahakikisha bei ya pipa la mafuta lazima ibaki kuwa zaidi ya dola 100 za Kimarekani, lakini mwaka huo huo walishindwa kupunguza uzalishaji wa mafuta na kufanya bei ya pipa moja iwe chini ya dola 50 za Kimarekani, kinyume na mpango wao wa awali wa kuweka bei juu ya hapo ili kupunguza matumizi ya mafuta.
Mwaka huu, nchi za Marekani na India ambazo ni watumiaji wakubwa wa mafuta zilijaribu kuishwishi OPEC kuongeza ugavi wa mafuta duniani ili kukabialiana na uhaba uliopo, OPEC hawajakubaliana na Marekani na India, hivyo mafuta yanaonekana kutofikia mahitaji ya ulimwengu na kupelekea bei kuwa juu.
2. Majanga ya Asili
Majanga yanaweza kusababisha bei za mafuta kupanda kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano, mwaka 2005 kimbunga cha Katrina kilipoikumba Marekani, usambazaji wa mafuta katika taifa hilo uliathirika kwa 20% na kusababisha bei za mafuta kupanda kwa dola 23.56 za Kimarekani.
Katika ulimwengu wa leo, kati ya majanga yaliyochangia sana kupanda kwa bei za mafuta ni janga la UVIKO-19 linaloikumba dunia yote.
> Bei mpya za mafuta mwezi Oktoba
3. Machafuko ya Kisiasa
Mwaka 2008, bei ya pipa la mafuta ilipanda hadi dola za Kimarekani 128, kufuatia vita nchini Afghanistan na Iraq. Mashariki ya Kati inazalisha sehemu kubwa ya mafuta yanayotumika duniani, vita katika eneo hilo huwa na athari katika bei ya mafuta.
Kwa sasa hali sio shwari nchini Afghanistan, japo hakuna takwimu za hivi karibuni kuonesha athari ya mchafuko hayo kwenye bei za mafuta, historia inaonesha kwamba vita katika nchi hizo inapelekea kupanda kwa bei ya mafuta.
4. Gharama za Uzalishaji
Gharama za uzalishaji wa mafuta zinatofautiana, uzalishaji katika nchi za Mashariki ya Kati ni wa gharama nafuu sana ukilinganisha na uzalishaji katika nchi kama Canada na Marekani. Uzalishaji katika zenye gharma ndogo za uzalishji unapoyumba, bei hupanda kwani mafuta yanayosambazwa hutoka katika nchi zenye gharama kubwa kiuzalishaji.
5. Ugavi na Mahitaji
Kanuni ya ugavi na mahitaji (Supply and Demand) huathiri sekta ya mafuta kama ilivyo kwa bidhaa nyingine. Kuna wakati ambapo dunia inahitaji zaidi kuliko kiwango kinachozalsihwa na kusambazwa na hivyo bei huwa juu. Wakati mwingine mafuta yanayozalishwa na kusambazwa huwa mengi kuliko kiasi kinachotajika na hivyo bei huwa chini, kama ilivyotokea mwaka 2014 ambapo nchi za Ulaya na China zilikuwa na mahitaji madogo ya mafuta wakati nchi za OPEC zinazalisha mafuta kwa wingi.