Klabu za Chelsea, Manchester City na Manchester United zipo kwenye kinyang’anyiro cha kumuwania mshambuliaji kinda wa Stoke City, Emre Tezgel (16) ambaye amekuwa akifananishwa na Harry Kane kutokana na uchezaji wake na uwezo wake wa kufunga mabao (Mail).
Paul Pogba ana ofa mpya mezani ya kuongeza mkataba kutoka klabu yake ya Manchester United tangu mwezi Julai mwaka huu. Licha ya mkataba huo ni wa muda mrefu wenye maboresho mapya na ongezeko kubwa la mshahara, lakini mpaka sasa hakuna muafaka uliofikiwa kutoka kwa Pogba na wakala wake Raiola. Man United wanasubiri uamuzi wake ambao wamekuwa wakishinikiza kwa miezi kadhaa sasa (Fabrizo Romano – Twitter).
Klabu ya Arsenal inawafuatilia wachezaji wawili wa England, Dominic Calvert-Lewin (24) na Ollie Watkins (25) lakini inakabiliwa na kibarua kigumu kutoka kwa Everton na Aston Villa (Sun). Lakini pia Arsenal bado wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Club Bruge Noa Lang (22) ambaye ananyatiwa pia na AC Milan ya Italia (Calciomercato, TEAMtalk).
Uwekezaji wa hisa zenye thamani ya pauni milioni 9.5 za klabu ya Manchester United zilizowekwa kwenye Soko la Hisa la New York na familia ya Glazer zimepanda hadi kufikia thamani ya pauni milioni 15.7 huku sababu ikitajwa kuwa ni ujio wa mshambuliaji wa Ureno mwenye umri wa miaka 36 Cristiano Ronaldo (Mail).
Kiungo wa kati wa England na Tottenham Harry Winks 25, yupo tayari kwa uhamisho wa mkopo kutoka kwenye klabu hiyo mwezi Januari na yuko radhi kwenda nje ya England (Times).
Vilabu vya Ligi kuu ya Englang vitapambana na Bayern Munich kumnasa kiungo wa kati wa Kijerumani Florian Wirtz anayekipiga Bayer Leverkusen (Fabrizio Romano).
Liverpool wanafikiria uhamisho wa mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, ambaye mazungumzo kuhusu mkataba wa mchezaji huyo (21) na Fiorentina yamevunjika (Mirror).
Borussia Dortmund wameamua kubaki na mshambuliaji wake Erling Haaland 21, mpaka mwaka 2023 (Sport Bild – German).
Hatma ya muda mrefu ya nyota wa PSG, Kylian Mbappe (22) bado inategemea klabu yake baada ya mazungumzo ya awali kati ya mama wa mchezaji huyo kukubaliana na mabingwa hao wa Ufaransa kuhusu mkataba mpya kwenda vizuri (RMC – AS).
Barcelona ipo tayari kumuachia beki wake Samuel Umtiti (27) dirisha dogo la usajili mwezi Januari. Mchezaji huyo ambaye hapati nafasi ya kucheza toka msimu mpya wa Laliga ulipofunguliwa msimu huu (Sport – Spanish).
#clickhabari