Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasihi vijana nchini kutotumia mitandao ya kijamii kwa mambo ya kiuhalifu badala yake watumie mitandao hiyo katika kukuza na kuleta maendeleo katika jamii.
Waziri Mkuu Majaliwa, amesema hayo alipotembelea baadhi ya mabanda katika viwanja vya Mazaina, Chato Mkoani Geita kwa ajili ya uzinduzi wa wiki ya Vijana Kitaifa.
> Serikali: Wafanyabiashara wadogo watengewe maeneo yanayofikika
“Mitandao ya kijamii na teknolojia ina uwezo mkubwa wa kuleta maendeleo katika jamii endapo mtaitumia vizuri kwani kuna vijana wengi wanaoendesha maisha yao kwa kutumia mitandao ya kijamii na teknolojia,” alisema Majaliwa.
Pia amewataka vijana kutumia fursa na rasilimali zilizopo kama ardhi yenye rutuba, vyanzo vya maji, mimea na madini na kuvihusisha kwenye teknolojia ili kuleta maendeleo.