Mambo 5 muhimu ya kufanya utokapo kwenye kazi hatarishi

HomeElimu

Mambo 5 muhimu ya kufanya utokapo kwenye kazi hatarishi

Mazingira hatarishi au ambayo si salama kwa mfanyakazi yanapunguza morali ya ufanyaji kazi lakini pia yanamfanya mhusika akose kujiamini. Mazingira ya kazi ambayo si salama yanaweza kusababishwa na uwepo wa unyanyasi wa kijinsia katika kazi, wafanyakazi kutopewa stahiki zao, kutoheshimiwa kwa mawazo ya wafanyakazi pamoja na kutokukuwa katika kazi kama kupandishwa cheo. Unapofanya kazi katika mazingira hayo unaweza kupata athari katika akili hivyo unapoenda kuanza kazi mpya fanya yafuatayo

1. Jipe muda wa kukaa na watu wengine
Kabla haujaanza kazi yako mpya tafuta muda kaa na watu ambao unawapenda inaweza ikawa familia yako au marafiki zako ili uweze kurudisha sehemu ya furaha yako na itakufanya ujione una thamani tofauti na mazingira uliyokuwepo awali. Unaweza pia kutembelea vivutio vya utalii ili  ‘ku-refresh’ akili yako.

2. Zungumzia changamoto ulizopitia
Tafuta mtu ambaye unamuamini ambaye anaweza kubeba changamoto zako kama zake lakini pia ambaye anaweza kukusikiliza na kukupa mawazo chanya. Wanasaikolojia wanaeleza kuwa kuzungumza kutakusaidia kupunguza mzigo wa maumivu ulioubeba ndani yako hiyo ni vizuri kuongea ili kuushusha huo. Kamwe usibebe maumivu ya kazi yako ya zamani kwenda nayo kwenye kazi yako mpya.

3. Jikumbushe kwamba wewe ni bora
Kila binadamu ana ubora wake katika kufanya jambo hivyo kama kwenye kazi yako ya zamani ulikua haupongezwi kwenye mafanikio uyapatayo basi usiumie, jikumbushe kuwa wewe ni bora na ubora wako hautegemei mawazo ya watu wengine. Jikumbushe kuwa ubora wako uko ndani yako hivyo unaweza kufanya vitu vikubwa zaidi kwenye sehemu yako mpya ya kazi.

4. Andaa mipango yako
Umeshafanya kazi katika mazingira ambayo si salama na unajua athari zake hivyo unatakiwa kuwa na malengo katika kazi yako mpya. Ainisha vitu vyote ambavyo ni ishara za kutokuwepo kwa usalama katika kazi yako ili ujue jinsi ya kukabiliana navyo kabla havijaanza kukuletea madhara ya kiakili na kimwili.

5. Jithamini mwenyewe
Fanya vitu ambavyo vitakupa furaha na amani, angalia vitu chanya, jiambie maneno mazuri ya kukujenga tafuta vitu vitakavyokusaidia kuwa bora katika ujuzi wako. Usikubali furaha yako itegemee mazingira au mtu jipe furaha wewe mwenyewe kwanza.

error: Content is protected !!