Katika kuhakikisha wannachi wanapata chanjo ya Uviko-19, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa watu kwenda kupata chanjo hiyo kwani badhi ya nchi Afrika zimeshaanza kupambana na wimbi la nne la ugonjwa huo na pia kupuuza wale wote wanaopotosha umma kwa maneno ya uongo kuhusu chanjo hiyo.
“Miongoni mwa hatua iliyochangia kupunguza maambukizi na visa vipya ya Uviko-19 ni chanjo. Jukumu la kinga ni la kila mmoja wetu, tunahitaji kuchukua tahadhari zaidi dhidi ya ugonjwa huu, sambamba na kuchanja,”
“Wapo Watanzania wanaulewa tofauti, natoa wito kuwadharau wanaopotosha umma kwa kuwataka wasichanje. Kuchanja ni hiari, lakini muhimu kwa sababu suala la afya ni la mtu mmoja.” alisema Majaliwa.
Waziri Mkuu aliyasema hayo alipokuwa akizindua mradi wa mapambano ya Uviko-19 unaotekelezwa na Kanisa Katoliki nchini, huku akitoa pongezi kwa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kwa kubuni utaratibu wa kujenga uhusiano na Marekani.